TANGAZO


Monday, October 1, 2012

Aliyekuwa Diwani wa CHADEMA ahamia CUF jijini Arusha



Aliyekuwa Diwani wa Chadema wa kata ya Elerai, Mkoani Arusha John Bayo, akitambulishwa na Profesa Lipumba mara baada ya kujiunga na Chama cha Wananchi (CUF), kwenye mkutano uliofanyika Mkoani Arusha jana, ambapo Chama hicho kinaendelea na kampeni yake ya Dira ya mabadiliko.
Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, akiwa kwenye mkutano huo jijini Arusha mwishoni mwa wiki.


Makamu wa Kwanza wa Rais wa Seriali ya Zanzibar, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), akihutubia mkutano wa chama hicho, uliofanyika jijini Arusha mwishoni mwa wiki.

Wapenzi na wanachama wa Chama cha Wananchi (CUF), wakiendelea kumsikiliza mgeni rasmi kwenye mkutano wa chama hicho, Mwenyekiti wa Chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba na katibu wake Mkuu, Maalim Seif Shariff Hamada, uliofanyika kwenye viwanja vya Levolosi, Halmashauri ya jiji la Arusha mwishoni mwa wiki (Picha zote na kamera yetu Arusha)

No comments:

Post a Comment