TANGAZO


Monday, October 1, 2012

Airtel yasherehekea uzinduzi Wiki ya Huduma kwa Wateja

 Meneja Huduma kwa Wateja wa Kampuni ya simu ya Airtel, Aneth Muga akitoa ufafanuzi kwa mmoja wa wateja waliotembelea duka la Moroco leo, ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja, inayoanza leo ambapo Airtel inasherehekea na kuwashukuru wateja wake nchi nzima. Pichani ni baadhi ya watoa huduma kwa wateja wa Airtel wakiwapatia huduma wateja wao.

 Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja, Adrian Lyamba (katikati), akiwaongoza wafanyakazi na wateja wa Airtel kukata keki, wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja, ambapo Airtel imejumuika na wateja wake katika kusherehekea na kukata keki pamoja na kuwashukuru kwa kutumia mtandao wa Airtel.

 Mmoja wa wateja wa Airtel, akimlisha keki Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja, Adrian Lyamba wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja, iliyofanyika Makao Makuu ya Airtel, jijini Dar es Salaam leo. (Picha zote na mdau wetu)

No comments:

Post a Comment