Baada ya mzozo wa kisheria wa miaka mingi, Mahakama kuu ya Uingereza imeamua kuwa Mhubiri wa Kiislamu mwenye siasa kali, Abu Hamza, na washukiwa wengine 4 watapelekwa Marekani kujibu mashtaka ya Ugaidi.
Kulingana na majaji, washukiwa hao watano watasafirishwa mara moja baada ya rufaa iliyowasilishwa na wakili wa Abu Hamza kupinga hatua hiyo kwa misingi ya kiafya kukataliwa.
Abu Hamza anahitajika nchini Marekani kujibu mashtaka ya kubuni kambi ya kigaidi katika eneo la Oregon.
Marekani imeridhishwa na uamuzi huo wa mahakama dhidi ya Abu Hamza aliyekuwa akitumikia kifungo cha miaka saba katika gereza la Uingereza kwa kutoa matamshi ya chuki.
No comments:
Post a Comment