Kikundi cha sarakasi kutoka nchini Ethiopia kijulikanacho kwa jina la Umoja kikionesha umahiri wake wa kucheza mtindo huo wakati sherehe za mahafali ya 23 yaliyoyofanyika jana katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni(TaSUBa), iliyopo Bagamoyo mkoani Pwani. Sherehe hizo ziliambatana na Tamasha la 31 la Sanaa na Utamaduni.
Mtoto mwenye umri wa miaka 4, Nyambuli Mganga akiwa na kikundi hicho cha sanaa na utamaduni cha Utandawazi Theatre Group Matwigha Chalo kutoka Nansole Ukerewe akionyesha umahiri wake wa kucheza ngoma ya Ukerewe inayojulikana kwa jina la Obusimbula katika meza kuu.
Mtoto Nyambuli Mganga akiwa na kikundi hicho, kutoka Nansole Ukerewe akionyesha umahiri wake wa kucheza ngoma ya Ukerewe inayojulikana kwa jina la Obusimbula kwa wahitimu katika sherehe za mahafali ya 23 ya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni(TaSUBa). Sherehe hizo ziliambatana na kilele cha maonesho ya 31 ya Tamasha na Sanaa na Utamaduni liliyofanyika katika ukumbi wa taasisi hiyo iliyopo Bagamoyo, mkoa wa Pwani. Nyambuli ambaye anarithi utamaduni huo kutoka kwa mama yake, Wiliherimina Kebela, ambaye yuko katika kikundi hicho.
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni (TaSuBa), Profesa Elias Jengo ambaye ni Mhadhiri wa taaluma hiyo, katika Chuo Kikuu cha Dares Salaam (UDSM), akimpatia cheti mhitimu wa Stashada ya Sanaa na Utamaduni , Charles Kiswaga katika mahafali ya 23 ya TaSUBa, yaliyofanyika kwenye ukumbi wa maonesho chuoni hapo. Katikati Mtendaji Mkuu wa taasisi hiyo Juma Bakari na kulia ni Mkuu wa Idara ya Taaluma Michael Kadinde.
Baadhi ya wahitimu wa Stashahada ya Juu ya Sanaa na Utamaduni wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasm Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni (TaSuBa), Profesa Elias Jengo (kushoto), ambaye ni Mhadhili wa taaluma hiyo katika Chuo Kikuu cha Dares Salaam (UDSM), aliyeko katikati ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Vijana, Profesa Hermas Mwansoko na kulia kwake ni Mtendaji Mkuu wa taasisi hiyo, Juma Bakari. Wengine ni baadhi ya wakufunzi. (Picha zote na Idara ya Habari, Maelezo)

No comments:
Post a Comment