TANGAZO


Saturday, September 29, 2012

Hafla ya kuchangia mfuko wa walemavu Zanzibar


Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko wa Serikali ya Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui, akitoa hotuba na maelezo kuhusu mfuko wa watu wenye ulemavu, katika hafla ya kuchangia mfuko huo, iliofanyika Zanzibar, hoteli ya Beach Ressort.
Baadhi ya wadau mbalimbali, wakipunga mikono kama ishara ya kupiga makofi kuwapongeza watu wenye ulemavu katika hafla ya kuchangia mfuko wa watu wenye ulemavu iliofanyika Zanzibar, Hoteli ya Beach Ressort.
Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein (katikati), akipunga mkono kama ishara ya kupiga makofi kwa lugha ya walemavu wa masikio (viziwi), katika hafla ya kuchangia mfuko wa watu wenye ulemavu iliofanyika Zanzibar, Hoteli ya Beach Ressort.
Wanafunzi wenye ulemavu wa macho kutoka Shule ya Msingi ya Kisiwandui na Sekondari ya Vikokotoni, Awena Hassan (kushoto) na Jamila Borafya (kulia), wakisoma utenzi katika hafla ya kuchangia mfuko wa watu wenye ulemavu iliofanyika Zanzibar, Hoteli ya Beach Ressort.
Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na wadau waliochangia kwa kiasi kikubwa mfuko wa watu wenye ulemavu katika hafla iliofanyika Zanzibar, Hoteli ya Beach Ressort.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akikabidhi picha yake, iliyochorwa na kuuzwa kwa shilingi za Kitanzania milioni moja  na nusu kwa Fortunata Temu wa  Swiss Port ya Dar es Salaam katika hafla ya kuchangia fedha kwa Mfuko wa watu wenye ulemavu Zanzibar, iliyofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Beach Resort, nje ya Mji wa Unguja. Kushoto ni Mwenyekiti wa mfuko huo, ambaye pia ni Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko, Nassor Ahmed Mazrui. (Picha na Ramadhan Othman, Ikulu)
Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, akimkabidhi Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Zahra Ali Hamad, picha ya Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Abeid Aman Karume, iliochorwa kwa mkono, ambayo imeuzwa shiling 1,200,000 katika hafla ya kuchangia mfuko wa watu wenye ulemavu, iliofanyika Zanzibar, Hoteli ya Beach Ressort.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akizindua Tovuti ya Mfuko wa Watu wenye Ulemavu, wakati wa hafla ya uchangishaji fedha kwa ajili ya mfuko huo jana, katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Beach Resort, nje ya Mji wa Unguja. (Picha na Ramadhan Othman, Ikulu)
Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein akipeana mikono na Ofisa uhusiano Mwandamizi wa NSSF, Theopista Muheta, aliempelekea Cheki ya Shiling milioni 10, katika hafla ya kuchangia mfuko wa watu wenye ulemavu, iliofanyika Zanzibar, Hoteli ya Beach Ressort. (Picha zote na Yussuf Simai - Maelezo Zanzibar)

No comments:

Post a Comment