Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein, akiwasili katika viwanja vya Salama Bwawani Hotel, kuhudhuria katika Futari iliyoandaliwa na Benki ya Watu wa
Zanzibar (PBZ), mjini Zanzibar leo na kupokelewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Benki hiyo, Mzee Abrahmani Mwinyijumbe (wapili kulia) na wa pili kushoto ni Meneja wa Benki, Juma Amour. (Picha zote na Ramadhan Othman, Ikulu)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Viongozi wa Dini ya Kiislamu, alipowasili katika viwanja vya Salama Bwawani Hotel, kuhudhuria katika Futari iliyoandaliwa na Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ), mjini Zanzibar leo. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Benki hiyo, Mzee Abrahmani Mwinyijumbe.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein, akichukua chakula wakati wa Futari iliyoandaliwa na Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) katika ukumbi wa Salama Bwawani Hotel, mjini Zanzibar leo pamoja na wananchi mbalimbali walihudhuria katika hafla hiyo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya watu wa Zanzibar (PBZ), Mzee Abrahmani Mwinyijumbe (kushoto) pamoja na viongozi wengine wakichukua chakula kwa ajili ya futari, iliyoandaliwa na Benki hiyo leo katika ukumbi wa Salama Bwawani mjini Zanzibar.
Viongozi mbalimbali wa Serikali, taasisi binafsi na wananchi wakichukua chakula cha futari iliyoandaliwa na Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ), ukumbi wa Salama Bwawani, mjini Zanzibar leo.
Baadhi ya akina mama walioalikwa katika futari iliyoandaliwa na Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) katika ukumbi wa Salama Bwawani, mjini Zanzibar leo, wakiwa katika harakati za uchuaji wa chakula kwa njia ya kupanga mstari, ikiwa ni utaratibu mzuri wa kujipatia chakula hicho.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein, akijumuika na viongozi wengine katika hafla ya chakula cha futari iliyoandaliwa na Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ), katika ukumbi wa Salama Bwawani Hotel mjini Zanzibar leo.
Baadhi ya wananchi na waumini wa Dini ya Kiislamu, wakiwa katika Futari iliyoandaliwa na Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ), hafla hiyo ilifanyika leo, katika ukumbi wa Salama Bwawani, mjini Zanzibar.
Baadhi ya wananchi na waumini wa Dini ya Kiislamu wakiwa katika Futari iliyoandaliwa na Benki ya Watu wa Zanzibar PBZ, katika ukumbi wa Salama Bwawani, mjini Zanzibar leo.
Baadhi ya wananchi na waumini wa Dini ya Kiislamu wakipata Futari iliyoandaliwa na Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) mjini Zanzibar leo.
Meneja wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ), Juma Amour, akitoa hutuba yake kwa niaba ya Benki hiyo na kueleza mikakati yao katika juhudi za kuboresha huduma za kiutendaji baada ya chakula cha futari, walichokiandaa na kuhudhuriwa na Rais wa Zanzibar, Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Salama, Hoteli ya Bwawani mjini humo leo.
No comments:
Post a Comment