Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Luteni mstaafu, Chiku Galawa akipeana mkono na Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Godwin Semunyo, wakati wa hafla ya kufuturisha iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wateja wake. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Tanga mjini, Halima Dendegu.
Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Godwin Semunyo (kulia), akiwa na baadhi ya Maofisa wa Benki hiyo wakati wa hafla hiyo ya futari.
Meneja wa benki ya CRDB, tawi la Tanga, Evarist Mnyele (kulia), akiwa na Maofisa wa Benki hiyo, wakati wa hafla ya kufuturisha, iliyofanyika jijini Tanga jana.
Baadhi ya wageni waalikwa wakipata futari.
|
Akina mama wakichukua chakula kilichoandaliwa kwa ajili ya futuri na benki ya CRDB, jijini Tanga jana. |
|
Ilikuwa ni futari ya nguvu iliyoandaliwa na CRDB, hapa vijana wakijisevia msosi. |
|
Wageni wakichukua msosi katika hafla hiyo ya futari iliyoandaliwa na benki ya CRDB, jijini Tanga jana. |
|
Vijana waalikwa wakichukua chukula kwa ajili ya kufuturu katika hafla hiyo, iliyoandalia na benki ya CRDB, jijini Tanga jana. |
|
Baadhi ya wageni waalikwa wakijichana kwa misosi hiyo, iliyoandaliwa na benki ya CRDB, jijini Tanga jana. |
|
Akina mama wakijichana kwa msosi huo, ulioandaliwa na benki ya CRDB, jijini Tanga jana. |
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Luteni mstaafu, Chiku Galawa (wa pili kushoto), akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Tanga mjini, Halima Dendegu (kushoto), wakati wa hafla ya kufuturisha iliyoandaliwa na benki ya CRDB kwa wateja wake na kufanyika kwenye Uwanja wa Mkwawani jijini Tanga.
Meneja wa CRDB, tawi la Tanga, Evarist Mnyele akizungumza wakati wa hafla ya kufuturisha, iliyoandaliwa na benki hiyo jijini Tanga jana. (Picha kwa hisani ya Habari Mseto Blog)
No comments:
Post a Comment