Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadik, muda mfupi baada ya kuwasili akitokea nchini Ghana ambapo alishiriki mazishi ya aliyekuwa Rais wa nchi hiyo, Marehemu John Atta Mills. Kushoto ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Davis Mwamunyange. (Picha na Freddy Maro).
Baadhi ya watoto yatima na walemavu wakishiriki katika futari, Ikulu jijini Dar es Salaam jana jioni.
Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, akisoma barua aliyoandikiwa na mtoto Khaitham Jumbe (kulia), wakati wa futari aliyowaandalia watoto wenye ulemavu na yatima, Ikulu jijini Dar es Salaam. Katikati anayeangalia ni mtoto Hamida Jacks, mdogo wake Khaitham. Mtoto Khaitham Jumbe ni mlemavu wa ngozi na alikuja Ikulu na wazazi wake.
Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, akigawa zawadi kwa watoto yatima na walemavu walohudhuria futari aliyowaandalia Ikulu, jijini Dar es Salaam jana jioni.
Mkewe wa Rais Kikwete, Mama Salma Kikwete, akigawa zawadi kwa watoto yatima na walemavu, waliohudhuria futari waliyoandalia na Rais Ikulu jijini Dar es Salaam jana jioni.
Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe, Mama Salma Kikwete, wakigawa zawadi kwa watoto yatima na walemavu waliohudhuria futari aliyowaandalia Ikulu jijini Dar es Salaam jana jioni.
No comments:
Post a Comment