Mmoja wa wafanyakazi wa mgahawa huo, Bakari Ally, akiwahudumia warembo hao.
Baadhi ya warembo wa Redd's Miss Ilala 2012, wakipata chakula kwenye Mgahawa mpya wa kisasa wa City Sports Lounge ambao ni moja ya wadhamini wa shindano hilo, litakalofanyika Septemba 7, 2012, katika ukumbi wa Nyumbani Lounge, wakati walipotembelea Ofisi za gazeti la Jambo Leo na mgahawa huo leo.
Mhariri wa michezo wa gazeti la Jambo Leo na Staa Spoti, Julius Kihampa, akiwapatia maelezo warembo hao, jinsi anavyoziandaa habari za michezo, walipokuwa wakitembelea Ofisi za gazeti hili jijini leo.
Baadhi ya warembo wa Redd's Miss Ilala 2012, wakiangalia baadhi ya nakala za gazeti la Jambo Leo wakati wa ziara hiyo leo.
Mmoja wa Wakurugenzi wa gazeti la Jambo Leo, Benny Kisaka akizungumza na warembo hao, wakati wa ziara hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Jambo Concepts, ambao inatoa magazeti ya Jambo Leo, Jambo Barand Tanzania na gazeti la michezo la Staa Spoti, Juma Pinto, akizungumza na warembo hao, kuhusu masuala mbalimbali ya kampuni hiyo, ambayo kupitia gazeti lake la Jambo Leo, imedhamini shindano hilo.
Mhariri Mkuu wa gazeti la Jambo Leo, Anistus Mwessa, akiwapatia maelezo warembo hao kuhusu utengenezwaji wa gazeti hilo. Aliyesimama kushoto ni mratibu wa shindano hilo kutoka kampuni ya Jambo Concepts, Juma Mabakila.
Baadhi ya warembo hao wakimsikiliza Mhariri huyo, wakati alipokuwa akiwapatia maelezo hayo. Aliyesimama kushoto ni mratibu wa shindano hilo kutoka Kampuni ya Jambo Concepts, Juma Mabakila.
Baadhi ya warembo hao, wakisikiliza kwa makini maelezo hayo yaliyokuwa yakitolewa na mhariri huyo, ofisini hapo leo.
Warembo wakiwa katika picha ya pamoja kwa ajili ya kumbukumbu nje ya Ofisi za gazeti la Jambo Leo.
Warembo wakipozi kwa picha ya pamoja kabla ya kuondoka baada ya kumaliza ziara yao hiyo. (Picha zote na Richard Mwaikenda)













No comments:
Post a Comment