TANGAZO


Thursday, August 23, 2012

Mashindano ya Safari Pool awamu ya Pili, Mkoa yazinduliwa Kawe leo

 Nahodha wa klabu ya Pool ya Jambo Lee, Kawe jijini Dar es Salaam,  Franco Daniel akicheza pool dhidi ya Judith Machajuku (kushoto) wa klabu hiyo, wakati walipopambana katika michezo ya ufunguzi wa mashindano ya Safari Pool, awamu ya pili, ngazi ya Mkoa, jijini jana. Katika mpambano huo Judith alimshinda nahodha wake, Daniel michezo 2-1. 

Judith Machajuku wa klabu ya Jambo Lee, Kawe jijini  Dar es Salaam, akicheza dhidi ya nahodha wake, Franco Daniel (kulia), wakati wa michezo ya ufunguzi wa mashindano ya Safari Pool, awamu ya pili, ngazi ya Mkoa, jijini leo.

Nahodha wa klabu ya Pool ya Jambo Lee, Kawe jijini Dar es Salaam, Franco Daniel akicheza pool dhidi ya Judith Machajuku wa klabu hiyo, wakati walipopambana katika ufunguzi wa mashindano ya Safari Pool, awamu ya pili, ngazi ya Mkoa, jijini leo.


Judith Machajuku wa klabu hiyo, akicheza mchezo huo dhidi ya mpinzani wake Franco Daniel, wakati wa michezo ya ufunguzi wa mashindano ya Safari Pool, awamu ya pili, ngazi ya Mkoa, jijini leo. 

Mchezaji Michael Kitendero wa klabu ya Jambo Lee, Kawe jijini Dar es Salaam, akicheza pool dhidi ya mpinzani wake, Judith Machajuku (kulia) wa klabu hiyo, wakati wa michezo ya ufunguzi wa mashindano ya Safari Pool, awamu ya pili, ngazi ya Mkoa, jijini leo. Kitendero, alishinda michezo 2-1. 

Judith Machajuku wa klabu Jambo Lee, akicheza dhidi ya Michael Kitendero wa klabu hiyo, wakati wa michezo ya ufunguzi wa mashindano ya Safari Pool, awamu ya pili, ngazi ya Mkoa, jijini Dar es Salaam leo. Kitendero, alishinda michezo 2-1. (Picha zote na Kassim Mbarouk)

No comments:

Post a Comment