Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akimkabidhi Tuzo ya Heshima msanii mstaafu wa muziki wa Taarab,
Mwanacha Hassan Kijole (65) wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi za
washindi wa Tuzo hizo za Wasanii bora wa muziki wa Zanzibar wa mwaka
2012, zilizodhaminiwa na Kampuni ya simu za mkononi ya Zantel.Hafla
hiyo ilifanyika jana usiku katika Ukumbi wa Hoteli ya Bwawani mjini
Zanzibar. Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Uzini na Mkurugenzi wa redio ya
Zenji Fm, Mohamed Seif Khatib (kushoto) ni Mkurugenzi wa Biashara wa
Kampuni ya Zantel, Zanzibar, Mohamed Baucha.
Baadhi ya wageni waalikwa na wadau wa sanaa, waliohudhuria hafla hiyo.
Baadhi ya wageni waalikwa na wadau wa sanaa, waliohudhuria hafla hiyo.
Mke
wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Zakhia
Bilal, akiwa ni miongoni mwa wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo.
Baadhi ya wageni waalikwa na wadau wa sanaa, waliohudhuria hafla hiyo.
Mkurugenzi
wa redio ya Briz Fm, bi. Mariam, akimkabidhi Tuzo ya kuwa msanii bora
wa Kike wa muziki wa Afro Pop, Msanii Baby J, wakati wa hafla ya
kukabidhi zawadi za washindi wa Tuzo hizo za Wasanii bora wa muziki wa
Zanzibar wa mwaka 2012, zilizodhaminiwa na Kampuni ya simu za mkononi ya
Zantel. Hafla hiyo ilifanyika jana katika Ukumbi wa Hoteli ya
Bwawani mjini Zanzibar.
Mkuu
wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Abdallah Mwinyi Mkuu, akimkabidhi Tuzo
mwanamuziki wa kundi la Taarab la Zanzibar One Modern Taarab, Saada
Nassor, baada ya kuibuka mshindo kwa kuwa Msanii bora wa Kike wa mwaka
wa muziki wa Taarab ya Kisasa, wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi za
washindi wa Tuzo hizo za Wasanii bora wa muziki wa Zanzibar wa mwaka
2012, zilizodhaminiwa na Kampuni ya simu za mkononi ya Zantel. Hafla
hiyo ilifanyika jana katika Ukumbi wa Hoteli ya Bwawani mjini Zanzibar.
Mbunge
wa Jimbo la Uzini na Mkurugenzi wa redio ya Zenji Fm, Mohamed Seif
Khatib, akimkabidhi Tuzo msanii, Rukia Ramadhan, aliyeibuka mshindi kwa
kuwa mwimbaji bora wa mwaka wa Taarab Aslia, wakati wa hafla ya
kukabidhi zawadi za washindi wa Tuzo hizo za Wasanii bora wa muziki wa
Zanzibar wa mwaka 2012, zilizodhaminiwa na Kampuni ya simu za mkononi
ya Zantel. Hafla hiyo ilifanyika jana katika Ukumbi wa Hoteli ya
Bwawani mjini Zanzibar.
Mwakilishi
wa Benki ya NBC kwa niaba ya Meneja wa benki hiyo, Asya Mohamed,
akimkabidhi tuzo ya kuwa na Studio bora ya mwaka 2012, Juma Mkuyumba 'Mk
Records', wakati wa hafla hiyo jana.
Ombeni
Swai, kutoka Kampuni ya Scannad ya jijini Dar es Salaam, akimkabidhi
Tuzo mmoja kati ya wasanii waliofanya vizuri mwaka 2012.
Abubakar
Liongo, akimkabidhi Tuzo msanii aliyefanya vizuri mwaka 2012, katika
muziki wa Hip Hop, Sabri Mshimba 'Chaby Six, wakati wa hafla hiyo.
Msanii Isma, akishambulia jukwaa wakati wa hafla hiyo.
Kundi la Dansi la Young Dancers, likishambulia jukwaa kwa burudani.
Msanii
aliyeibuka kidedea katika kategoli ya Muziki wa Afro Pop, Rashid
Khalfan Ali 'Dogo Fanni' akitembea kwa madaha kuelekea jukwaani
kukabidhiwa tuzo yake wakati wa hafla hiyo.
Baadhi ya wageni waalikwa na wadau wa sanaa, waliohudhuria hafla hiyo.
Mwakilishi
wa Jimbo la Raha Leo, Salim Nassor, akimkabidhi tuzo ya Msanii Bora
Chipukizi wa mwaka, msanii Emma Score, wakati wa hafla ya kukabidhi
zawadi za washindi wa Tuzo hizo za Wasanii bora wa muziki wa Zanzibar wa
mwaka 2012, zilizodhaminiwa na Kampuni ya simu za mkononi ya Zantel.
Hafla hiyo ilifanyika jana katika Ukumbi wa Hoteli ya Bwawani mjini
Zanzibar.
Picha ya pamoja baada ya zoezi la kukabidhi zawadi kwa washindi wa tuzo hizo. (Picha na Muhidin Sufiani)
No comments:
Post a Comment