TANGAZO


Saturday, July 7, 2012

Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) yanyakua tuzo Maonesho ya Sabasaba

Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Balozi Seif Ali Idi akimkabidhi Cheti pamojo na tuzo Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Shaban Mrisho baada ya kampuni hiyo kuibuka washindi katika kipengele cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kwenye Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Dar es Salaam.
 

 Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), wakiwa katika picha ya pamoja na Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Shaban Mrisho katika Maonyesho ya Sabasaba, Kilwa Road Dar es Salaam leo.
 
Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya TTCL, wakipiga picha ya kumbukumbu wakati wa maonesho ya Kimataifa ya Biashara, Kilwa Road, Dar es Salaam leo.
Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Amanda Luhanga akitoa ufafanuzi wa huduma wanazotoa kwa watu waliofika katika banda la TCCL wakati wa Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika barabara ya Kilwa, Dar es Salaam.
 
Wafanyakazi wa TTCL, wakiwahudumia wananchi waliofika kwenye banda lao katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara, barabara ya Kilwa Dar es Salaam leo.
Ofisa Masoko wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Thomas Lemunge akielezea faida za mkongo wa Taifa wa Mawasiliano kwa watu waliotembelea banda la TTCL.
 
Mmoja wa wafanyakazi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), akiwapatia maelezo wananchi waliofika kwenye banda la kampuni hiyo kwenye maonesho ya Kimatifa ya Biashara, Viwanja vya Malimu Nyererwe, Kilwa Road, Dar es Salaam leo.
 
Ofisa Masoko wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Thomas Lemunge akiwaonyesha watu waliotembelea banda la TTCL Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano, kwenye maonesho hayo leo. (Picha zote na Francis Dande)

No comments:

Post a Comment