TANGAZO


Monday, June 4, 2012

Waziri Kagasheki awa mgeni rasmi Mahafali ya Askari wa Wanayapori

Mshauri wa mafunzo ya Ulinzi wa Chuo cha Taasisi ya wanyamapori cha Pasiansi, Mwanza, Venance Tossi (kushoto), akifuatilia jambo katika sherehe za mahafali ya 47 ya wahitimu wa chuo hicho, ngazi ya Stashahada na Astashahada.

Mkuu wa Chuo cha Taasisi ya Wanyamapori ya Pasiansi, Lowaeli Damalu, akitoa taarifa ya Chuo kwa Waziri wa Mali Asili na Utalii, Balozi Hamis Kagasheki (wa pili kushoto). Wa pili kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Paul Sarakikya.




Mwenyekiti Cathbert Nahonya, akisoma risala kwa Waziri wa Mali Asili na Utalii, Balozi Hamis Kagasheki (wa pili kushoto), wakati wa mahafali kuhayo. Kulia ni Mkuu wa chuo hicho Lowaeli Damalu.

Wanafunzi wa Shule ya Mazoezi ya Butimba, wakiimba nyimbo ya kutunza mazingiara na kulinda wanyamapori mbele ya Waziri wa Mali Asili na Utalii, Balozi Hamis Kagasheki katika sherehe za mahafali ya 47 ya chuo cha Taasisi ya Wanaymapori cha Pasiansi Mwanza jana.



Balozi Hamis Kagasheki, ambaye ni Waziri wa Mali Asili na Utalii, akimtunuku cheti mmoja wa wahtimu wa mafunzo ya askari wa wanyamapori katika ngazi ya Astashahada na Shahada.

Wanafunzi wa Shule ya Wasichana Ngaza, wakiimba wimbo kuhusu kutunza mazingiara na wanyamapori katika mahafali ya 47 ya chuo cha taasisi ya wanyamapori cha Pasansi Mwanza.


Waziri wa Mali Asli na Utalii, Balozi Hamis Kagasheki, akizungumza kabla ya kufunga mafunzo ya wahitimu wa kozi ya askari wa wanayamapori katika ngazi ya Astashahada na Stashahada jana. kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Paul Sarakikya .


Waziri wa Mali Asili na Utalii, Balozi Hamis Kagasheki (katikati) akiteta jambo la Mwenyekiti wa Bodi ya chuo cha Taasisi ya Wanyamapori cha Pasinsi Mwanza, Catbert Nahonya muda mfupi bada ya kufunga mafunzo kwa wahitimu 166  wa chuo hicho katika ngazi ya Stashahada na Astashahada jana.

Waziri wa Mali Asili na Utalii, Balozi Hamis  Kagasheki, akiwa katika picha ya pamoja na wahitimu wa mafunzo ya askari wa wanyamapori katika chuo cha taasisis hiyo cha Pasiansi Mwanza.



Balozi Hamis Kagasheki, aliyeshika magoti, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya  wahitimu wa mafunzo ya askari wa wanyamapori katika ngazi ya Astashahada na Stashahada muda mfupi baada ya kuwakabidhi vyeti wahitimu 166 kwenye mahafali ya 47 ya chuo hicho. Wahimu 86 hawakupewa vyeti na wametakiwa kurudia mitihani baada ya kushindwa kufaulu. Kushoto kwa Kagasheki ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya wanyamapori, Paul Sarakikya na kulia kwake ni Mwenyekiti wa Bodi ya chuo cha wanyamapori Pasiansi, Cathbert Nahonya. (Picha zote na Baltazar Mashaka, Mwanza)


No comments:

Post a Comment