TANGAZO


Sunday, June 24, 2012

Tanzania, China zasherehekea maendeleo ya teknolojia ya Kilimo

Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Eng. Christopher Chiza (kulia), akizungumza jambo na Balozi wa China nchini Tanzania, Lu Youqing, wakati wa hafla fupi ya kusherehekea   mafanikio ya matumizi ya teknolojia ya kilimo kati ya China na Tanzania kwenye miradi mbalimbali ya kilimo nchini, jijini Dar es Salaam leo.


Viongozi mbalimbali kutoka Ubalozi wa China na Serikali ya Tanzania, wakiimba wimbo wa Taifa wa Tanzania kabla ya kuanza hafla fupi ya kusherehekea mafanikio ya matumizi ya teknolojia ya kilimo kati ya China na Tanzania kwenye miradi mbalimbali inayofanyika nchini Tanzania. Kutoka kushoto nyuma ni balozi wa China nchini Tanzania, Lu Youqing, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa, Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Eng. Christopher Chiza na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, John Haule.


Baadhi ya mashuhuda wa miradi mbalimbali ya ushirikiano kati ya China na Tanzania ukiwemo ujenzi wa  Reli ya Uhuru (TAZARA), walioalikwa kwenye hafla hiyo, Abdul Haji na  Roza Kangoma, ambaye ni mama wa Balozi wa Zambia nchini Tanzania pia aliwahi kuwa Mkuu wa Chuo cha Mafunzo cha TAZARA.



Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Eng. Christopher Chiza, akizungumza na wageni mbalimbali walioalikwa na Ubalozi wa China nchini Tanzania, kuhusu  mikakati ya Serikali ya kuboresha kilimo na kuongeza uzalishaji wa mazao, wakati wa hafla fupi ya kusherehekea   mafanikio ya matumizi ya teknolojia ya kilimo kati ya China na Tanzania katika miradi mbalimbali ya Kilimo inayofanyika Tanzania, Dar es Salaam leo.


Wageni mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo katika Ubalozi wa China nchini Tanzania wakifuatilia masuala mbalimbali yaliyokuwa yakitendeka wakati wa hafla hiyo.


Raia kutoka Mataifa mbalimbali, waliohudhuria katika hafla hiyo fupi ya kusherehekea   mafanikio ya matumizi ya teknolojia ya kilimo kutoka nchini China katika miradi mbalimbali inayofanyika nchini Tanzania, wakijipatia nakala mbalimbali za machapisho kuhusu shughuli za kilimo, siasa, Utamaduni, Teknolojia na masuala ya kijamii. (Picha na Aron Msigwa -MAELEZO)

No comments:

Post a Comment