Redds Miss Higher learning 2011, Jackline Kinabo (aliyekaa), ambaye amemaliza muda wake, akiwa tayari kumvalisha taji, mshindi wa Miss Redd's Higher Learning 2012 katika ukumbi wa Kilimani lilikofanyika shindano hilo, usiku wa kuamkia leo.
Mshindi wa Taji la Redd's Miss Higher Learning, Dodoma Mwaka 2012, Virginia Mokili (katikakati), akiwa katika picha ya pamoja na mshindi wa pili wa taji hilo, Jenipher Mafuru (kulia) na mshindi wa tatu, Lilian Maleo (kushoto) mara baada ya Shindano Kumalizika.
Baadhi ya washiriki wa Shindano la kumsaka kimwana wa Redd's, Elimu ya juu, Kanda ya Dodoma, wakiwa katika picha ya pamoja kabla warembo kuchujwa katika hatua ya tano bora.
| Mmoja wa washiriki wa shindano la kumsaka mrembo wa Redd's Miss Higher learning Kanda ya Dodoma, akipozi la vazi la usiku, wakati walipokuwa wakipita kwenye jukwa hilo, usiku wa kuamkia leo. |
Mmoja wa washiriki wa Shindano la kumsaka mlimbwende wa Redd's Miss Higher Learning Kanda ya Dodoma 2012, akipita kwa madaha na vazi la ufukweni.
Jaji Mkuu wa Shindano la Kumsaka Mlimbwende wa Redds Elimu ya Juu Kanda ya Dodoma, akisoma majina ya washiriki waliobahatika kuingia hatua ya tano bora.
Warembo waliofanikiwa kuingia hatua ya tano bora, wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya hatua ya mwisho ya kujibu mwaswali kwa ajili ya kumpata kisura wa shindano hilo.
Mmoja wa washiriki wa shindano hilo, akichagua swali, wakati wa hatua ya mwisho ya shindano hilo.
| Msanii Barnaba Elias akitumbuiza kwenye onesho hilo la kumtafuta Redd's Miss Higher Learnig 2012, Dodoma, usiku wa kuamkia leo. |
Msanii wa Kizazi Kipya, Barnaba Elias, akiwashirikisha mashabiki wakati alipokuwa akitoa burudani katika shindano hilo la kumsaka mlimbwende wa Redd's Elimu ya Juu Kanda ya Dodoma 2012, Ukumbi wa Kilimani, usiku wa kuamkia leo.
Afisa Utamaduni wa Manispaa ya Dodoma, Kishosha akimkabidhi zawadi mshindi wa Kwanza wa Taji la Redd's, Miss Higher Learning Dodoma 2012, Virginia Mokiri, mara baada ya kuibuka mshindi wa kwanza wa shindano hilo.
Mshindi wa Pili wa taji la Redd's, Miss Higher Learning, Dodoma 2012, Jennipher Mafuru, akipokea zawadi yake kutoka kwa Afisa Utamaduni wa Manispaa ya Dodoma, Kishosha mara baada ya kuibuka mshindi wa pili wa shindano hilo.
Mshindi wa tatu wa taji la Redd's Miss Higher Learning Dodoma 2012, Lilian Maleo akikabidhiwa zawadi ya king'amuzi kutoka Kampuni ya StarTime na Afisa Utamaduni wa Manispaa ya Dodoma.
Walimbwende walioshiriki katika kinyang'anyiro cha kumsaka Redds Miss Higher Learning Dodoma 2012, wakicheza shoo, wakati wa kuanza kinyang'anyiro hicho, kilichofanyika katika ukumbi wa Kilimani.
Baadhi ya watazamaji wakifuatilia mpambano huo.
|
Baadhi ya watazamaji waliojitokeza kushuhudia nani ataibuka mshindi wa taji hilo usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa Kilimani wakiangalia kwa makini shindano hilo.
|
Baadhi ya watazamaji waliojitokeza kushuhudia nani ataibuka mshindi wa taji hilo wakifuatilia kwa makini shindano hilo.
|
Baadhi ya watazamaji waliojitokeza wakifuatilia hatua mbalimbali walizokuw waskishindana warembo hao.
Washiriki wote wa kuwania Taji la Miss Higher Learning Dodoma 2012 wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wadhamini wa shindano hilo lililofanyika Katika Ukumbi wa Kilimani huku Virginia Mokiri Kuibuka MShindi wa Taji hilo. (Picha Zote na Josephat Lukaza wa lukaza.blogspot.com)

No comments:
Post a Comment