TANGAZO


Wednesday, May 2, 2012

Tahadhari kwa wachezaji Euro 2012


Pierluigi Collina
Pierluigi Collina
Wachezaji wanaomzonga mwamuzi wakati wa mechi kupinga maamuzi kwenye mashindano ya fainali za Kombe la Mataifa ya Euro 2012 watarajie hatua kali, ameonya refa mkongwe Pierluigi Collina.
Luigi amesema kua tabia hiyo inatoa sura mbaya kwa mchezo wa kandanda, amesema mwamuzi huyo aliyestaafu kupuliza kipenga mnamo mwaka 2005 na hivi sasa ni afisa mwandamizi wa masuala ya waamuzi wa UEFA.
Kumzonga refa ni kosa
Kumzonga refa ni kosa
Ameongezea kusema kua, wachezaji watafahamishwa kua kumzonga refa hakuruhusiwi, na waamuzi wanafahamu vyema kua watakapozongwa na wachezaji, ruhusa ipo ya kutoa kadi za njano, moja au hata zaidi, aliwambia wandishi wa habari mjini Warsaw, mji mkuu wa mashindano ya Euro 2012 nchini Poland.
Collina amesema kua wachezaji pia wataonywa na kuadhibiwa endapo watazidi kushiriki malumbano na wachezaji wa upinzani.
Mizozano baina ya wachezaji ni suala ambalo tunataka lipigwe marufuku uwanjani. Hatutakia kuona wachezaji 20 wakianza malumbano. Wachezaji wenyewe wanafahamu, na hili si geni kwao, kwamba inapotokea malumbano uwanjani na kushiriki zaidi ya wachezaji kumi, kadi ya manjano sharti ionyeshwe.
Kumzonga refa ni kosa
Kumzonga refa ni kosa
Takriban jumla ya waamuzi 80 walioteuliwa na UEFA kwa ajili ya mashindano ya Ulaya nchini Poland na Ukraine wanahudhuria kisomo cha wiki nzima mjini Warsaw. Hawa ni pamoja na waamuzi kutoka England, Ufaransa,Ujerumani, Uholanzi, Hungary, Italia,Ureno,Scotland, Slovenia, Uhispania, Sweden na Uturuki.
Collina amesema kua wanafanya mazowezi ya mwili na visomo vikali vya uwanjani na kiakili kusaidia katika kufikia maamuzi mazuri na sawa wakati wa mashindano hususan juu ya kuchezeana vibaya.
Mojapo ya malengo ya yanayokusudiwa kufikiwa ndani ya viwanja ni kuwalinda wachezaji. Nidhamu pia ni sehemu ya ulinzi wa wachezaji.
Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Ulaya ya Euro 2012, yatakayoanza tarehe 8 Juni ndiyo mwanzo wa mpango wa UEFA kuendelea kujaribu matumizi ya maamuzi yasiyorisha kwa kutumia maofisa 8.

No comments:

Post a Comment