TANGAZO


Tuesday, May 22, 2012

Rais Kikwete, amuapisha Waziri Profesa Mwandosya, Kazi Maalum


Rais Jakaya Kikwete (kushoto), akimwapisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalumu), Profesa Mark Mwandosya katika hafla iliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam leo asubuhi. (Picha zote na Kamanda Mwaikenda)

 Profesa Mark Mwandosya, akila kiapo cha Utiifu kwa Rais na Serikali yake pia kuwa mwaminifu katika kazi yake ya Uwaziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Kazi Maalumu, Ikulu Dar es Salaam leo.

Profesa Mwandosya, ambaye ni Mbunge wa Rungwe Mashariki, akitia saini kwenye kiapo chake hicho, mbele ya Rais Jakaya Kikwete.
Rais Kikwete akitia saini kwenye kiapo hicho.

                                                        Rais Jakaya Kikwete akitia saini kwenye hati za kiapo hicho.
Rais Jakaya Kikwete akimkabidhi vifaa vya kufanyia kazi (Muongozo), Profesa Mwandosya baada ya kumuapisha leo Ikulu.

 Profesa Mwandosya akiwa amekaa na mkewe Lucy, akisubiri kuapishwa na Rais Jakaya Kikwete Ikulu, Dar es Salaam leo.

 Profesa Mwandosya akiwa na baadhi ya ndugu na jamaa walioalikwa kushuhudia sherehe za kuapishwa kwake Ikulu.

 Wageni waalikwa, wakishuhudia Profesa Mark Mwandosya, akiapishwa na Rais Jakaya Kikwete, Ikulu jijini leo.

 Profesa Mwandosya akielekea eneo la kuapishwa, mara baada ya Rais Kikwete kufika kwenye ukumbi huo wa Ikulu kwa ajili ya kutekeleza kiapo hicho.

 Profesa Mark Mwandosya, akiwa tayari kwa ajili ya kuapishwa na Rais Jakaya Kikwete.

Profesa Mwandosya akielekezwa jambo na mmoja wa Maofisa wa Ikulu, wakati wa kiapo hicho.

Rais Jakaya Kikwete, akiwa amemshikilia Waziri wa Nchi katika Ofisi yake, Kazi Maalum, Mark Mwandosya kwa ajili ya kwenda kupiga picha za kumbukumbu mara baada ya kumuapisha. 

 Rais Jakaya Kikwete na Waziri Profesa Mark Mwandosya, wakiwa katika picha ya pamoja na ndugu, jamaa wa familia baada ya shughuli ya kuapishwa kumalizika.

Rais Jakaya Kikwete akimuonesha kitu, Waziri wa Nchi katika Ofisi yake, Kazi Maalum, Profesa Mark Mwandosya wakati wa kupiga picha za kumbukumbu baada ya kumwapisha.
Wandishi wa habari, wakiwa wamelizingira gari la Waziri Profesa Mark Mwandosya, wakitaka kuzungumza naye baada ya kumalizika kwa shughuli mbaimbali za kuapishwa, Ikulu Dar es Salaam leo

No comments:

Post a Comment