TANGAZO


Tuesday, May 22, 2012

Dk. Bilal azindua kitabu cha 'Cheklist Of Tanzanian Species'

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kitabu cha ‘Checklist Of Tanzanian Species’, katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo Mei 22, 2012. (Picha na Muhidin Sufiani-OMR)


 Baadhi ya wadau waliohudhulia hafla hiyo, wakimsikiliza Makamu wa Rais, Dk. Gharib Mohamed Bilala, wakati alipokuwa akizungumza kwenye uzinduzi huo.

Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe, ili kuzindua rasmi kitabu cha ‘Checklist Of Tanzanian Species’, wakati wa hafla hiyo, iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo Mei 22, 2012. Kushoto ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa. Makame Mbarawa na wa pili kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech), Dk. Hassan Mshinda. 


Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akikionesha kitabu cha ‘Checklist Of Tanzanian Species’, baada ya  kukizindua rasmi katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa na kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech), Dk. Hassan Mshinda.


 Baadhi ya wadau, waliohudhuria katika hafla hiyo, wakifuatilia uzinduzi wa kitabu hicho, ukumbini hapo leo. 


Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akimsikiliza Meneja wa Shirika la TANBIF Node, Hulda Gideon, wakati alipotembelea sehemu ya maonesho yaliyoandaliwa na Shirika hilo, kwenye uzinduzi wa kitabu cha ‘Checklist Of Tanzanian Species’, uliofanyika leo Mei 22, 2012 jijini Dar es Salaam.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na wadau waliohudhuria uzinduzi huo.

No comments:

Post a Comment