TANGAZO


Saturday, May 19, 2012

Mbunge Zungu, atembelea Mashina ya CCM, Pamba Road, Mama na Baba Lishe, Kivukoni

Katibu wa Uchumi na Fedha Kata ya Kivukoni, Abdallah Ally 'Malema wa Tanzania', akimpatia maelezo Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Azzan 'Zungu', (kulia), wakati alipokuwa katika ziara ya kuwashukuru na kuwasikiliza shida zao, wapiga kura wake kwenye mashina leo jijini Dar es Salaam, ambapo alimweza kuhusu nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), zilizopo karibu na Vyuo Vikuu kwamba wapewe wanafunzi kama hostel, ili kupunguza kero za wanafunzi, kuepukana na kulala kwenye kwenye hosteli zilizoko kwenye mabaa.

 Mwenyekiti wa Shina la Pamba Road, Said Masanga, akimpatia maelezo Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan 'Zungu', wakati alipowatembelea kwa ajili ya kuwashukuru na kuwasikiliza shida zao leo. Kusho aliyesimama ni Katibu wa Uchumi na Fedha Kata ya Kivukoni, Abdallah Ally Isere 'Malema'.

Mbunge Mussa Azzan 'Zungu', akifafanua jambo kwa wanachama wa Shina hilo, wakati alipofika kwenye shina hilo leo kwa ajili ya kuwashukuru wapiga kura wake na kuwasikiliza shida zao. Kushoto ni Mjumbe wa shina hilo, Saleh Ndonoo na Kulia ni Mwenyekiti wa shina, Said Masanga.

 Baadhi ya wanachama wa Shina hilo, wakimsikiliza Mbunge wao, Mussa Zungu wakati alipokuwa akizungumza nao leo.

 Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kata ya Kivukoni Peter Mbawala, akizungumza wakati alipokuwa akimpatia taarifa Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Zungu (kushoto), alipotembelea shina la Pamba Road kwa ajili ya kuwashukuru na kuwasikiliza shida zao wapiga kura wake hao leo. Katikati ni Mwenyekiti wa shina hilo, Said Masanga.

Baadhi ya wanachama wa Shina hilo, wakiwa wamemzukguka Mbunge wao, Mussa Zungu, ili kumsikiliza wakati alipokuwa akizungumza nao kwenye shina lao la Barabara ya Pamba, jijini Dar es Salaam, kwenye ziara yake ya kuyatembelea mashina ya Chama hicho, kwenye Jimbo lake la Ilala.

Mbunge Mussa Azzan 'Zungu', akizungumza na wanachama wa Shina la Pamba Road, Kataya Kivukoni, wakati wa ziara yake ya kuwashukuru na kuwasikiliza shida zao, wapiga kura wake hao, Dar es Salaam leo.

Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Azzan 'Zungu', akiwasili kwenye maeneo ya Shina la Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mama na Baba lishe ,Kata ya Kivukoni, Dar es Salaam kwa ajili ya kuwashukuru na kuwasikiliza shida zao katika maeneo yao ya kazi leo.

 Baadhi ya wanachama wa Shina namba 12 la Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mama na Baba lishe, Kata ya Kivukoni, Dar es Salaam, wakimshangilia Mbunge wao, Mussa Azzan Zungu wakati akiwasili kwenye tawi lao hilo kwa ajili ya kuwashukuru na kuwasikiliza shida zao.

 Mwenyekitiwa Elizabeth Nyasuru wa Shina namba 12 la Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mama na Baba lishe, Kata ya Kivukoni, Dar es Salaam, akimkaribisha Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan Zungu wakati akilpofika kwenye tawi hilo kwa ajili ya kuwashukuru na kuwasikiliza shida zao.

 Mwanachama wa Shina namba 12 la Mama na Baba Lishe, Kata ya Kivukoni, Stahamili Kongoi, akisoma risala ya shina hilo, mbele ya Mbunge Zungu (kulia), wakati alipowatembelea kwa ajili ya kuwashukuru wapiga kura wake kwenye shina hilo leo. Katikati ni Mwenyekiti wa CCM Kata ya Kivukoni, Peter Mbawala.

 Mwanachama wa Shina namba 12 la Mama na Baba Lishe, Kata ya Kivukoni, Maraki Mwita, akimweleza Mbunge Zungu, matatizo wanayokabiliana nayo kwenye sehemu yao ya kazi wakati wa ziara ya Mbunge huyo kwenye shina hilo leo.

Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Azzan 'Zungu', akizungumza na wanachama wa Shina namaba 12 la Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mama na Baba lishe, Kata ya Kivukoni, Dar es Salaam leo, wakati alipofika kwenye shina hilo, kwa ajili ya kuwashukuru na kuwasikiliza shida zao.

 Mwenyekiti wa Vikoba wa shina namba 12 la Mama na Baba Lishe, Kata ya Kivukoni, jijini Dar es Salaam, Zena Mohammed, akifurahia baada ya kukabidhiwa sh. 500,000 na Mbunge Zungu kwa ajili ya kutunisha mfuko wao huo.

 Wanachama wa shina namba 12 la Mama na Baba Lishe, Kata ya Kivukoni jijini, wakimuaga Mbunge wao, Mussa Azzan Zungu baada ya kumaliza kuzungumza nao leo kwenye shina lao hilo, wakati alipofanya ziara ya kuwashukuru na kusikiliza shida zao katika eneo lao la kazi leo.

No comments:

Post a Comment