Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal. Akisoma hotuba yake wakati akiufungua mkutano huo, Chuo kipya cha Jeshi (NDC), kilichojengwa na Wachina eneo la Kunduchi jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi kutoka kwa Liutenant General wa Jeshi la Bangladesh, M F Akbar, baada ya kuufungua rasmi mkutano wa siku nne wa kubadilishana uzoefu baina ya Serikali ya Tanzania na China, kuhusu mafunzo ya Ulinzi leo Mei 21, 2012 katika Chuo kipya cha Jeshi, Kunduchi jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi kutoka kwa Meja General Charles Lawrence Makakala, baada ya kuufungua rasmi mkutano wa siku nne wa kubadilishana uzoefu baina ya Serikali ya Tanzania na China, kuhusu mafunzo ya Ulinzi, Chuo kipya cha Jeshi Kunduchi jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo, wakiwa katika ukumbi wa mkutano wakati Makamu wa Rais Dk. Bilal akiufungua mkutano huo leo.
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo, wakibadilisha mawazo wakati walipokuwa wakifuatilia hotuba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, wakati alipokuwa akiufungua mkutano huo.
Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano huo mara baada ya kuufungua rasmi leo.
Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowasa, wakati akiondoka katika Chuo cha Mafunzo ya Jeshi cha National Defence College (NDC), baada ya ufunguzi wa mkutano wa siku nne wa kubadilishana uzoefu baina ya Serikali ya Tanzania na China, kuhusu mafunzo ya Ulinzi, Kunduchi jijini Dar es Salaam.









No comments:
Post a Comment