Roberto Di Matteo
Meneja wa mda wa Chelsea Roberto di Matteo alipoingia mkutano
wa wandishi wa habari kwa mazungumzo ya baada ya mechi saa saba na robo usiku wa
manane, akijivunia rekodi kubwa kwa meneja yeyote wa mda kuwahi kushinda,
machungu ya Chelsea daima kukosa Kombe la Ligi ya mabingwa tayari yalikua
yamefutwa kwa dawa nyepesi kutamka, Ushindi.
Didier Drogba
Hili lilifuatiwa na Drogba kuvua shati lake na kulipeperusha juu ya kichwa
chake kuonyesha furaha ya ushindi baada ya kukimbia kuzunguka uwanja mzima, huku
Fernando Torres na David Luiz wakipanda juu ya besera la goli kuonyesha furaha
yao. Wakati huo Mmiliki wa klabu hio Abramovich mwenyewe akiruka na kupiga
makofi huku akiimba ikidhihirisha sura isiyoonekana kwa kawaida kwa mtu msiri
asiyeonyesha hisia zake.
Ikiwa mkwaju huo ulikua wa mwisho kwa mchezaji huyu kutoka Ivory Coast kama
mchezaji wa Chelsea, pamoja na bao lake la kusawazisha lile la Thomas Mueller,
basi Drogba ataondoka kwa kuandikisha rekodi yake binafsi.Drogba mwenyewe hakuweza kuelezea bayana juu ya majaliwa yake baada ya kukabidhiwa zawadi ya mchezaji bora wa mechi hio ya fainali ya Ligi ya mabingwa barani Ulaya. Punde mkataba wake unafikia mwisho na bado hakuna matumaini ya kama ataongezewa mda.
Hatma ya Meneja wa mda Di Matteo bado haijabainika na mwenyewe alishindwa kusema ni nini alidokezewa na Abramovich walipokumbatiana kwenye ngazi kabla ya sherehe za kukabidhiwa Kombe kwa mara ya kwanza katika historia ya miaka 107 ya klabu hio.
Abramovich
Mara pekee kwa klabu hii kushamiri katika mashindano ya Ulaya, ulikua mwaka 1971 kabla ya hata Liverpool kushinda nje ya England, Chelsea ilipoichapa Real Madrid na kujishindia Kombe la Mshindi la mwaka huo wa 1971.
Drogba, aliongoza na kua kinara, na hivyo kuandika jina lake kwa vitendo katika historia. Kipa Petr Cech amepitia kipindi kigumu wakati wa kampeni ya Ligi ya mabingwa wa Ulaya lakini mjini Munich alionyesha ukomavu kwa kuzuia mkwaju wa Arjen Robben katika kipindi cha ziada na wakati wa matuta alizuia mkwaju wa Ivica Olic.
Andre Villas Boas na Di Matteo
Matokeo ya Napoli yakageuka kuipendelea Chelsea na baada ya hapo kuichabanga Benfica kujishindia fursa ya kukutana na Barcelona ambayo waliweza kuishinda kwa hatua zote mbili,nyumbani na ugenini licha ya kusukumwa kwa dakika nyingi.
Sifa kubwa anastahili Roberto Di Matteo aliyechimba ndani ya bongo za wachezaji aliyewafahamu na kuamini kua wana uwezo wa kushiriki na kucheza soka kwa kiwango cha juu na kushinda.
Bila shaka wadadisi watakosoa mbinu zilizotumiwa dhidi ya Barcelona na huko Munich lakini jibu la Di Matteo ni moja tu angalia rekodi ya mwaka 2012, Mabingwa wa Ulaya ni Chelsea.

No comments:
Post a Comment