TANGAZO


Saturday, May 12, 2012

Chama cha Maendeleo ya Watu wa Muheza (MDTF), chapata uongozi mpya

Mwenyekiti aliyemaliza muda wake wa Chama cha Maendeleo ya Watu wa Muheza (MDTF), Tido Mhando, akizungumza na wanachama wa chama hicho, wakati wa Mkutano Mkuu, uliofanyika jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya kuwachagua viongozi wake wapya. Wa pili kushoto ni Mgeni rasmi wa mkutano huo, Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Alshaymar Kweygir akiteta jambo na mmoja wa wajumbe wa kamati ya uongozi, Rose Lugendo na kulia ni Mkurugenzi wa Chama, Clement Mang'enya. (Picha zote na Kassim Mbarouk)


Msimamizi wa uchaguzi wa Chama cha Maendeleo ya Watu wa Muheza (MDTF), Mohamed Kaungwa, akielezea taratibu za uchaguzi huo, utakavyoendeshwa kwa ajili ya kuwapata viongozi wapya wa kukiongoza chama hicho. Wa pili kushoto ni Mgeni rasmi wa mkutano huo, Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Alshaymar Kweygir, mjumbe wa kamati ya uongozi, Rose Lugendo (wa kwanza kushoto), Mwenyekiti wa MDTF, aliyemaliza muda wake, Tido Mhando na kulia ni Mkurugenzi wa Chama, Clement Mang'enya.


Baadhi ya wanachama wa Chama hicho wakiwa kwenye mkutano huo, ukumbi wa Kanisa la Anglikana la Mtakatifu Albano, Posta mpya, jijini Dar es Salaam leo, wakifuatilia maelezo mbalimbali yaliyokuwa yakitolewa.

Mmoja wa wagombea wa uongozi katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti, Mwanaidi Ngoda, akijielezea kwa ajili ya kuomba kura kwa wajumbe, ili kupata ridhaa ya kukiongoza chama hicho.


Mwanachama Twaha Msenga, akizungumza katika mkutano huo, kuomba kura kwa wajumbe kwa ajili kugombea nafasi ya Katibu Mkuu wa Chama cha MDTF.


Mkurugenzi wa Chama, Clement Mang'enya, akitoa ufafanuzi kwa wajumbe wa mkutano huo, wakati wa kupiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa kuwapata viongozi wapya wa Chama hicho.
Ramadhan Semtawa wa Gazeti la Mwananchi, akijieleza kwa wanachama wa MDTF kwa ajili ya kuomba kura katika nafasi ya Katibu Mwenezi wa chama.

Mwanachama Mariam Chambika, akizungumza katika mkutano huo, wakati wa kujieleza kwa wanachama kwa ajili ya kupata kura zitakazo mwezesha kuchaguliwa kwa nafasi ya mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Chama hicho.


Gregory Mgaya, akijieleza mbele ya wanachama wa Chama hicho, kutaka ridhaa ya kuwa mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Chama.


Mwaimu Mtangi, akizungumza wakati wa kuomba kura za wajumbe wa mkutano huo kwa ajili ya nafasi ya mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Chama.


Mwenyekiti aliyemaliza muda wake wa Chama cha Maendeleo ya Watu wa Muheza (MDTF), Tido Mhando, akizungumza baada ya kukamilika kwa uchaguzi, ili kuwashukuru wajumbe kwa kufanikisha uchaguzi huo pamoja na ushirikiano alioupata wakati wa uongozi wake. Pia aliukaribisha uongozi huo mpya kwenye meza kuu na kuwakabidhi nakala ya Katiba ya  chama kwa ajili ya kuanza kazi mara moja.

Mwenyekiti mstaafu wa Chama cha Maendeleo ya Watu wa Muheza (MDTF), Tido Mhando (kulia), akimkabidhi Mwenyekiti mpya, Nicholaus Mgaya Katiba ya Chama hicho, baada ya kuchaguliwa kukiongoza chama hicho leo.
Mwenyekiti mpya, Nicholaus Mgaya, akizungumza na wanachama katika mkutano huo, kutoa shukurani zake kwa kumchagua kukiongoza Chama hicho. Wa pili kushoto ni Makamu Mwenyekiti, Mwanaidi Ngoda, Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Alshaymar Kweygir, ambaye ni mgeni rasmi na mjumbe wa kamati ya uongozi, Rose Lugendo (wa kwanza kushoto), wakiwa meza kuu.

Mgeni rasmi, Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Alshaymar Kweygir, akizungumza baada ya kuchaguliwa uongozi mpya wa Chama cha MDTF na kuutaka uongozi huo, kufanyakazi bila woga na kujituma kwa ajili ya kuwaletea maendeleo watu wa Muheza.
Unogozi mpya wa Chama cha Maendeleo ya Watu wa Muheza, ukiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Alshymar Kwegyir (wa pili kushoto) na Mwenyekiti aliyemaliza muda wake, Tido Mhando.
Uogozi mpya wa Chama cha Maendeleo ya Watu wa Muheza, ukiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika uchaguzi huo.

No comments:

Post a Comment