kuhusu utendaji kazi wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) katika ukumbi wa mikutano wa Wizara hiyo, uliopo jijini Dar es Salaam. Siku za hivi karibuni utendaji kazi wa TAZARA ulikuwa wa kusuasua kutokana na matatizo mbalimbali yanayolikabili Shirika hilo. (Picha na Anna Nkinda - Maelezo)
Baadhi ya viongozi wa Umoja wa Wafanyakazi wa Reli Tanzania (TRAWU), tawi la TAZARA, wakijadili mambo mbalimbali mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa utendaji kazi wa Mamlaka ya TAZARA baina ya Waziri wa Uchukuzi, Omari Nundu na waandishi wa habari, uliofanyika leo, jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya viongozi wa Umoja wa Wafanyakazi wa Reli Tanzania (TRAWU), tawi la TAZARA wakisikiliza jambo kutoka kwa Lufingo Mwanghba (kulia), mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa utendaji kazi wa Mamlaka ya TAZARA baina ya Waziri wa Uchukuzi Omari Nundu na waandishi wa habari, uliofanyika leo, jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya watendaji wakuu wa wizara ya Uchukuzi ,wakimsikiliza Waziri Omari Nundu (hayupo pichani), wakati akizungu na waandishi wa habari, kuhusiana na utendaji kazi wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA), leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mhandisi Omari Chambo.
No comments:
Post a Comment