Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akiangalia jiko bunifu kwenye jiko la shule ya Sekondari ya Kishapu akiwa katika ziara ya Wilaya ya Kishapu, mkoani Shinyanga, Februari 23, 2012. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kishapu, wakicheza ngoma wakati Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alipofungua jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu akiwa katika ziara ya Mkoa wa Shinyanga jana.
Askari wa Jeshi la Jadi (Sungusungu) wa mji mdogo wa Maganzo, wakicheza ngoma yao, wakati Waziri Mkuu Mizengo Pinda, alipowasili kwa ajili ya mkutano wa hadhara katika mji huo, akiwa katika ziara ya Mkoa wa Shinyanga Februari 23,2012.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akiwapungia kwa ajili ya kuwaaga wananchi wa mji mdogo wa Maganzo, baada ya kuwahutubia akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Shinyanga.
No comments:
Post a Comment