Wachezaji wa Simba, wakiwa katika mazoezi ya kujiandaa kwa mpambano wao wa marudiano na Kiyovu ya Rwanda katika Kombe la Shirikisho barani, mchezo utakaochezwa mwishoni mwa wiki ijayo, jijini Dar es Salaam. (Picha na Kassim Mbarouk)
Kocha wa Simba, Cirkovic Milovan (kushoto), akiwafuatilia wachezaji wa timu hiyo, wakati walipokuwa wakifanya mazoezi, uwanja wa Sigara, Dar es Salaam leo, kujiandaa kwa ajili ya pambano lao la marudiano na Kiyovu FC ya Rwanda, katika michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika, mchezo utakapigwa Uwanja wa Taifa, jijini mwishoni mwa wiki ijayo.
Kocha wa Simba, Cirkovic Milovan, akimpigia mpira mmoja wa wachezaji waliopandishwa kutoka timu B ya kikosi hicho, wakati wa mazoezi hayo leo jioni, Uwanja wa Sigara, Chang'ombe, jijini Dar es Salaam.
Wachezaji wa Simba, wakikimbia kwa ajili ya kupasha misuli kabla ya kuanza mazoezi ya nguvu, Uwanja wa Sigara, Chang'ombe jijini leo jioni. Kesho kikosi hicho kitajitupa Uwanja wa Taifa, kupambana na Azam FC ya jijini.
No comments:
Post a Comment