TANGAZO


Monday, February 27, 2012

Makamu wa Rais Dk. Bilal, atembelea na kuzindua mradi wa umwagiliajiI Rungwe.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea na kukagua mtaro wa kupitishia maji ya umwagiliaji katika kilimo cha mradi uliopo kijiji cha Kisegese, wakati akiwa katika siku yake ya mwisho ya ziara yake ya Mkoa wa Mbeya jana, Februari 26, 2012. (Picha na Muhidin Sufiani-OMR)


 Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiweka jiwe la msingi katika chanzo cha mradi wa maji ya umwagiliaji wa hicho, wenye urefu wa km 7, wakati akiwa katika siku ya mwisho ya ziara yake, mkoani Mbeya jana.


 Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, wakiangalia mpunga katika eneo la shamba darasa, lililopo kijiji cha Kisegese wilayani Rungwe jana.


 Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akipokea  mkuki kutoka kwa mwakilishi wa wazee wa kabila la Wanyakyusa wa kijiji cha Mbambo wilayani  Rungwe, Ambakisye Mwakatobe, ikiwa ni ishara ya kumkabidhi wadhifa wa kuwa Mzee wa Kabila la Wanyakyusa, wakati wa ziara hiyo, alipofika katika Kijiji hicho kuwahutubia wananchi. Kulia ni mkewe,  mama Asha Bilal.



Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiwa na mkuki na vazi rasmi la heshima la kabila la Wanyakyusa, baada ya kukabidhiwa wadhifa huo na wazee wa kabila la hilo katika kijiji Mbambo wilayani  Rungwe, Mbeya jana Februri 26, 2012. 

No comments:

Post a Comment