Afisa Mawasiliano wa Kampuni ya Airtel, Dangio Kaniki akimpongeza mmoja wa washindi wa shindano la Nani Mkali, Daniel Mshana, baada ya kusaini fomu ya kuthibitisha ushindi baada ya kujishindia pesa taslimu sh. milioni moja katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya Airtel, leo Februari 27. Kulia ni Afisa Uhusiano wa Kampuni ya Airtel, Jane Matinde.
Mmoja wa washindi wa promosheni hiyo, Daniel Mshana (katikati), akiongea na waandishi wa habari, baada ya kukabidhiwa kitita cha sh. milioni moja baada ya kuibuka kuwa mshindi wa wiki ya kwanza ya promosheni ya nani mkali.
No comments:
Post a Comment