Korea Kaskania imesema kuwa imefanikiwa kulifanyia jaribio bomu la nyuklia ambalo linaweza kuwekwa kwenye kombora la masafa marefu.
Taifa hilo la koministi lilisema jaribio hilo la sita la bomu la nyuklia, lilifanikiwa saa kadhaa baada ya mitetemeko mitatu kutambuliwa.
Korea Kaskazini ilisema ililifanyia jaribio bomu la haidrojeni, kifaa ambacho kina nguvu zaidi kuliko bomu la nyuklia.
Wadadisi wanasema kuwa kuna ishara kuwa uwezo wa nyuklia wa Korea Kaskazini unazidi kukua.
- Mzozo wa Korea Kaskazini na Marekani kwa muktasari
- China 'yaeleza wasiwasi' kuhusu Korea Kaskazini
- Marekani: Hatutaivumilia tena Korea Kaskazini
Watabiri wa hali ya hewa mapema walitambua tetemeo dogo la ardhi, eneo ambapo Korea Kaskazini ilikuwa imefanyia majaribio ya nyuklia awali.
Tetemeko hilo dogo lilitokea saa kadha baada ya kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un kupigwa picha akiwa na kile ambacho vyombo vya habari vilisema kuwa lilikua ni aina mpya ya bomu la hydrogen.

Vyombo vya habari vilisema kuwa kifaa hicho kinaweza kutundikwa kwenye kombora la masafa marefu.
Korea Kusini ilisema kuwa tetemeo hilo la ardhi lilitokea katika kaunti ya Kilju, lilipo eneo la kufanyia majaribio ya nyuklia la Punggye-ri.
- China yataka Marekani na Korea Kaskazini kuvumiliana
- Wamarekani kupigwa 'marufuku kuzuru Korea Kaskazini'
- 'Kifaa' cha Korea Kaskazini chashambuliwa na K. Kusini
Muda baadaye Rais wa Korea Kaskazini Moon Jae-in aliita mkutanao wa dharura wa baraza lake la usalama wa taifa.
Ripoti za awali kutoka kwa idara ya hali ya hewa ya Marekani zilitaja tetemeko hilo kuwa la ukubwa kwa 5.6 lakini baadaye likasema kuwa ukubwa huo ni wa 6.3 katika vipimo vya richa.

No comments:
Post a Comment