Rais wa Marekani Donald Trump na kikosi chake cha usalama wa taifa watafanya mkutano baadaye leo, kujadili jaribio la hivi punde la nyuklia lililofanywa na Korea Kaskazini, kwa mujibu wa taarifa kutoka Ikulu ya White House.
Hii ni baada ya Trump kujibu hatua ya Korea Kaskazini ya kulifanyia jaribio bomu hilo la nyuklia.
"Matamshi ya nchi hiyo na vitendo vyake vinandelea kuwa vyenye hatari kubwa kwa Marekani," Trump aliandika kwenye mtandao wa twitter.
- Trump: Korea Kaskazini watakuwa kwenye 'shida kubwa'
- Trump: Korea Kaskazini imeanza kutuheshimu
- Trump: tutaidhibiti Korea Kaskazini
Trump pia amezilaumua China na Korea Kaskazini kuhusu jinsi zinavyoishughulikia Korea Kaskazini.
"Korea Kaskazini imekuwa tisho na uibu kwa China," ambaye ni mshirika wake na ambaye amekuwa na mafanikio kidogo katika kupata suluhu.
"Matamshi ya kufurahisha ya Korea Kusini kwa Korea Kaskazini hayatafaulu," Trump alisema.
Wakati huo huo watu kwenye mji mkuu wa Korea Kaskazini Pyongyang, wanaendelea kufahamu hatua ya nchi yao ya kulifanyia jaribio bomu la nyuklia.
Watu hao walipigwa picha wakisherehekea hatua hiyo.




No comments:
Post a Comment