Karibu watu 65,000 wakazi wa mji Frankfurt wamendoka makwao kutoa nafasi kwa wataalamu wanaoharibu bomu kubwa ambalo lilikosa kulipuka wakati wa vita vya pilia vya dunia.
Polisi wanasema kuwa shughuli ya kuharibu bomu hilo ilianza kufuatia kuhamishwa watu wengi zaidi katika historia ya Ujerumani baada ya vita.
Maeneo yaliyohamishwa watu ni pamoja na hospitali, makao ya watu wazee na benki kuu ya Ujerumani.

Inaaminika kwa kuna maelfu ya mabomu ambayo hayakulipuka nchini Ujerumani.
Wenyeji wengi walisema kuwa wangetumia muda wao mwingi siku ya leo kutembelea familia, kuzuru sehemu tofauti za mjii hadi itakapobainika kuwa eneo hilo liko salama.

Polisi walivyambia vyombo vya habari kuwa shughuliya kuwahamisha watu ilikuwa imepangwa na kwamba kila mtu alikuwa ameondolewa eneo hatari.
- Wakazi 70,000 kuhamishwa Frankfurt kwa sababu ya bomu kubwa
- China 'yaeleza wasiwasi' kuhusu Korea Kaskazini
Bomu hilo la tani 1.4 la Uingezea, lilipatikana katika sehemu moja ya ujenzi siku ya Jumatano.


No comments:
Post a Comment