TANGAZO


Sunday, July 16, 2017

Rais Erdogan awasifu waliozima mapinduzi ya kijeshi Uturuki

President Erdogan addresses the crowd in Istanbul

Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionRais Erdogan awasifu waliozima mapinduzi ya kijeshi Uturuki
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, amehudhuria mkutano mmoja mkuu wa makumi kwa maelfu ya watu, nje ya majengo ya Bunge mjini Ankara, katika maadhimisho ya mwaka wa kwanza ya jaribio la mapinduzi ya kijeshi, yaliyotibuka mwaka jana.
Maadhimisho hayo yanajumuisha pia sauti na video za shambulio lililotokea, kwenye majengo ya bunge, ambalo lilitekelezwa na vikosi vya waasi.
Bwana Erdogan amewasifia, wanasiasa waliopinga jaribio hilo, kuacha majengo ya bunge yakiwa wazi na kulaani mashambulio ya angani.
Awali katika jiji kuu la Istanbul, Bwana Erdogan, aliuambia umati mkubwa wa watu kuwa raia wako radhi, kufanya kila wawezalo ili kulinda Uturuki.
Ameunga mkono hatua ya kuwashika watu kiholela, tangu kutibuka kwa jaribio hilo la mapinduzi, ambapo watu 250 waliuwawa-huku akiongeza kuwa hakutakuwa na huruma na waliopanga mapinduzi hayo.
Amesema kwamba inafaa wote wakatwe vichwa- Mara Bunge la nchi hiyo likipitisha hukumu ya kifo.
Wapinzani wa Bwana Erdogan, hawakuhudhuria maadhimisho hayo.
Tens of thousands went to the bridge in Istanbul that has become a landmark of the failed coupHaki miliki ya pichaEPA
Image captionRais Erdogan awasifu waliozima mapinduzi ya kijeshi Uturuki

No comments:

Post a Comment