Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho amesema kuwa kuna uwezekano mkubwa Zlatan Ibrahimovic ambaye hana mkataba na klabu hiyo akapewa kandarasi mpya.
Mshambuliaji huyo wa Sweden mwenye umri wa miaka 35 aliachiliwa huru baada ya kukosa kandarasi mpya.
Amekuwa akipona upasuaiji wa jeraha la goti katika uwanja wa mazoezi wa Old Trafford.
Mourinho: Iwapo uamuzi ni kusalia na kusubiri hadi Disemba -hawezi kurudi hivyobasi kwa nini tusubiri? Tunazungumza na kubadilisha mawazo.
Ibrahimovic alitia saini kandarasi ya mwaka mmoja mnamo mwezi Julai 2016, lakini hakongezewa kandarasi baada ya kupata jeraha lililomaliza msimu wake mnamo mwezi Aprili.
Alifunga mabao 28 katika mechi 46 katika mashindano yote ya United.
Mourinho pia alisema anataka kuwasajili mmoja ama wachezaji wawili msimu huu.
No comments:
Post a Comment