TANGAZO


Saturday, July 15, 2017

BALOZI SEIF IDDI AFANYA MAHOJIANO NA WANAHABARI WA KITUO CHA TELEVISHENI CHA KIMATAIFA CHINA OFISINI KWAKE VUGA MJINI ZANZIBAR

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Timu ya Wanahabari wa Kituo cha Matangazo ya Televisheni cha Kimataifa cha China (CCTV), iliyofika Ofisini kwake kumfanyia Mahojiano Maalum.(Picha zote na Hassan Issa – OMPR – ZNZ)
Balozi Seif akimkaribisha Mtampta wa Timu ya Wanahabari wa CCTV aliyepo katika Kitengo cha Madaktari wa China  waliopo Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Bwana Zhou Ziyue (maarufu – Juma). 
Timu ya Wanahabari wa CCTV ikimpongeza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwa kukubali ombi lao la kumfanyia Mahojiano Maalum kuhusu Historia ya Madaktari wa China wanaotoa huduma Zanzibar tokea miaka ya 60.
Mhadhiri wa Chuo Kukuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) wa Lugha ya Kichina Profesa Li  Xany Alice kushoto  akimpongeza Balozi Seif kwa kukamilisha vyema Mahojiano yao.   
Timu ya Wanahabari wa Kituo cha Matangazo ya Televisheni cha Kimataifa cha China (CCTV)  ikiwa kazini kuchukuwa Picha ya Mahojiano baina ya Wanahabari wa Kituo hicho na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi. 
Balozi Seif akifurahia zawadi nzuri alizopewa kama ukumbusho kutoka kwa Timu ya Wanahabari wa Kituo cha Matangazo ya Televisheni cha Kimataifa cha China (CCTV) baada ya kumaliza Mahojiano yao. 
Balozi Seif akifurahia zawadi nzuri alizopewa kama ukumbusho kutoka kwa Timu ya Wanahabari wa Kituo cha Matangazo ya Televisheni cha Kimataifa cha China (CCTV) baada ya kumaliza Mahojiano yao. 
Balozi Seif akifurahia zawadi nzuri alizopewa kama ukumbusho kutoka kwa Timu ya Wanahabari wa Kituo cha Matangazo ya Televisheni cha Kimataifa cha China (CCTV) baada ya kumaliza Mahojiano yao. 
Balozi Seif akipiga picha na wanahabari wa Kituo cha Matangazo ya Televisheni cha Kimataifa cha China (CCTV) baada ya kumaliza Mahojiano yao. 
Balozi Seif akipiga picha na wanahabari wa Kituo cha Matangazo ya Televisheni cha Kimataifa cha China (CCTV) baada ya kumaliza Mahojiano yao. 
Balozi Seif akipiga picha na wanahabari wa Kituo cha Matangazo ya Televisheni cha Kimataifa cha China (CCTV) baada ya kumaliza Mahojiano yao.

Na Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
15/7/2017.
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameipongeza Serikali ya Jamuhuri ya Watu wa China kwa uamuzi wake wa kujitolea kwa dhati wa kuiunga mkono Tanzania na Zanzibar  katika kusaidia Taaluma na Huduma kwenye Sekta ya Afya.

Amesema mchango wa China katika sekta hiyo umewezesha Wananchi walio wengi Nchini kujihisi kwamba Wataalamu na Madaktari  hao wa Kichina wanaotoa huduma za afya Nchini kama ni miongoni mwa Ndugu zao wanaoshirikiana katika maisha ya Kawaida Mitaani.

Balozi Seif Ali Iddi alitoa pongezi hizo hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar wakati akihojiwa na Wanahabari wa Kituo cha Matangazo ya Televisheni cha Kimataifa Cha China (CCTV), ambapo wanahabari hao wapo Zanzibar kufanya kipindi Maalum kinachohusu Historia ya Madaktari wa China wanaotoa huduma za Afya kwa Takriban Mikaka 53 iliyopita.

Alisema Wananchi wa Zanzibar kwa kipindi kirefu wamekuwa na ukaribu na Madaktari wa Kichina kutokana na Wataalamu na Mabingwa hao mahiri katika utendaji kazi wao kuzingatia zaidi maadili yaliyowawezesha kujenga sifa na Heshima kubwa.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwahakikishia Wanahabari  hao wa Kituo cha Matangazo ya Televisheni ya CCTV kwamba  Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kushirikiana na China katika kuona malengo ya ushirikiano yaliyofikiwa kati ya pande hizo mbili karibu Miaka 53 iliyopita nyuma yanafanikiwa ipasavyo.

Akizungumzia ushirikiano wa Kiuchumi na Kijamii  uliopo kati  ya China na Bara la Afrika Balozi Seif alisema yapo mafungamano mazuri yaliyofikiwa kupitia Mpango Maalum ulioanzishwa wa China – Africa ambao tayari umeshaanza kuleta mafanikio.

Alisema ushirikiano wa Kiuchumi na Kitaalamu ambao China imejikubalisha kusaidia zaidi Taaluma  Kwenye Mataifa ya Bara la Afrika umesaidia kuibua Wataalamu wa Kizalendo katika Mataifa hayo ambao wameanza kusaidia nguvu za uzalishaji unaozingatia Teknolojia ya Kisasa.

Balozi Seif alifahamisha kwamba miradi ya Maendeleo hasa katika sekta za Miundombinu ya Mawasiliano, Afya, Kilimo, Utamaduni, Michezo na hata shughuli za Kijamii chini ya usimamizi wa Mabingwa na Wataalamu wa China imeanza kushuhudiwa ikipiga hatua kubwa za maendeleo.

Hata hivyo Balozi Seif aliielezea Timu hiyo ya Wanahabari wa CCTV kwamba China bado ina safari ndefu ya kuendelea kulisaidia  Kitaaluma Bara la Afrika katika  azma ya Bara hilo ya kujikomboa  na umaskini hasa kwa Mataifa ya Jangwa la Sahara.

No comments:

Post a Comment