Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amekuwa akimtumia ujumbe mfupi wa maandishi Alexis Sanchez, 28, kujaribu kumshawishi asiondoke Emirates. (Sun)
Mshambuliaji wa Monaco Kylian Mbappe ameonesha dalili za kuondoka katika klabu yake hiyo huku Arsenal wakiendelea kumnyatia. (Marca)
Chelsea wana uhakika wa kuwapiku Liverpool katika kumsajili Pierre Emerick-Aubameyang, 28, kutoka Borussia Dortmund, ambao sasa wameanza mazungumzo ya kumtaka Olivier Giroud wa Arsenal. (Daily Mirror)
Nemanja Matic, 28, huenda akajiunga na Juventus baada ya Chelsea kumruhusu kutojiunga na kikosi kinachokwenda China na Singapore kwa ajili ya mechi za kujiandaa na msimu mpya. Diego Costa pia ameachwa. (Guardian)
Arsenal wameonesha dalili za kumtaka Nemanja Matic, na wapo tayari kubadilishana na Alex Oxlade-Chamberlain, 23. (Calcio Mercato)
Kasper Schmeichel, 30, amepata matumaini ya kujiunga na Manchester United baada ya taarifa kuwa Real Madrid wamepanda dau la kumtaka David de Gea, 26. (Daily Mirror)
Manchester United wana uhakika Real Madrid hawataiweza bei ya David de Gea. (ESPN)
Iwapo David de Gea atakwenda Real Madrid, meneja wa Manchester United atataka mchezaji mmoja kutoka Real na huenda akamtaka beki Rafael Varane. (Don Balon)
Kipa namba tatu wa Manchester United, Joel Pereira, 21, ana nafasi ya kuwa namba moja iwapo De Gea ataondoka. (Independent)
Inter Milan huenda wakamuulizia mshambuliaji wa Manchester United Anthony Martial wamchukue kwa mkopo kama sehemu ya mkataba wa United kumsajili Ivan Perisic, 28. (Daily Telegraph)
Tottenham watachuana na Juventus katika kumsajili beki wa Porto Ricardo Pereira, na watatazamiwa kulipa pauni milioni 22, kumchukua mchezaji huyo kuziba pengo la Kyle Walker. (Evening Standard)
Joe Hart anakaribia kukamilisha usajili wake wa pauni milioni 10 kutoka Manchester City kwenda West Ham. (Manchester Evening News)
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho hatoishutumu bodi ya klabu kwa kushindwa kumsajili Alvaro Morata. (Daily Express)
Liverpool huenda wakapanda dau la pauni milioni 65 kutaka kumsajili kiungo wa RB Leipzig Naby Keita, 22. (Liverpool Echo)
Roma wanajiandaa kupanda dau la pauni milioni 30 kumtaka winga wa Leicester Riyad Mahrez, 26. (Goal)
Meneja wa Birmingham Harry Redknapp anataka kumsajili beki wa zamani wa Arsenal na Chelsea, Ashley Cole, 36, kutoka LA Galaxy. (Sun)
Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara zitakapothibitishwa. Kwa orodha kamili ya wachezaji waliokamilisha rasmi usajili bofya link hii: http://www.bbc.co.uk/sport/football/transfers
Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Jumamosi njema.
No comments:
Post a Comment