Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akizungumza wakati wa mkutano na Kampuni zinazojihusisha na Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asilia Nchini uliofanyikia Madimba, mkoani Mtwara hivi karibuni. Kushoto ni Kaimu Kamishna Msaidizi wa Nishati Sehemu ya Petroli, Mwanamani Kidaya.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (mbele katikati) akiongoza mkutano na wawakilishi wa Kampuni za Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asilia Nchini.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Mhandisi Kapuulya Musomba (wa pili kulia), akizungumza wakati wa mkutano. Kulia ni Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.
Baadhi ya wawakilishi wa Kampuni za Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asilia Nchini kwenye mkutano na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (hayupo pichani).
Mwakilishi kutoka Kampuni ya Ophir Energy, Halfan Halfan (katikati) akielezea maendeleo ya shughuli zinazofanywa na kampuni yake wakati wa mkutano wa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) na Kampuni za Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asilia nchini.
Baadhi ya wawakilishi wa Kampuni za Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asilia Nchini kwenye mkutano na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (hayupo pichani).
Na Mohamed Saif, Nishati na Madini
WAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amesema mikutano ya kila baada ya miezi mitatu na Kampuni zinazojihusisha na Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asilia Nchini itakuwa ikifanyika katika maeneo mbalimbali nchini hususan kwenye rasilimali husika.
Waziri Muhongo aliyasema hayo hivi karibuni Mkoani Mtwara wakati wa mkutano wake na wawakilishi wa kampuni hizo uliofanyikia kwenye Kituo cha Kuchakata Gesi Asilia cha Madimba.
Alisema mikutano husika ilikua ikifanyikia jijini Dar es Salaam lakini ili kuleta tija zaidi, imeamuliwa iwe inafanyikia kwenye maeneo yenye gesi asilia na baadaye siku za usoni itafanyika kwenye maeneo yatakayogundulika kuwa na mafuta.
Aliongeza kuwa kila baada ya miezi mitatu kumekuwepo na utaratibu wa kukutana kwa ajili ya kutathmini tmaendeleo ya miradi husika na kila kampuni inawasilisha ratiba yake ya kazi ambayo inajadiliwa.
“Hii mikutano kila kampuni inatupatia ratiba yake ya kazi, tunaijadili na tunashauriana na kama wana matatizo tunatafuta suluhisho,” alisema Waziri Muhongo.
Waziri Muhongo alisema shughuli za Utafutaji, Uvunaji na Uendelezaji wa Gesi Asilia na Mafuta zinaendelea vizuri huku majadiliano mbalimbali yakiendelea kuhusiana na utekelezaji wa miradi husika.
No comments:
Post a Comment