Wachezaji wa kulipwa nchini Argentina wamepiga kura ya kufanya mgomo wikendi hii katika mzozo kuhusu malipo yao.
Baadhi ya wachezaji wanadai malimbikizi ya mishara ya miezi mitano ambayo hawajalipwa na vilabu vyao, na muungano wao unasema kuwa madeni hayo ni sharti yalipwe kabla ya mechi za ligi kuendelea.
Hatua hii inajiri baada ya mwanzo wa msimu huu kutatizwa na mzozo mwengine kati ya shirikisho la soka nchini humo na serikali kuhusiana na haki za runinga kuonyesha mchezo huo .
Mzozo huo umetatuliwa lakini wachezaji wanasema kuwa fedha hizo hazijawafikia.
Shirikisho la soka nchini humo limetishia kuzipiga faini klabu kubwa ambazo hazitawasilisha timu zao katika mechi.
No comments:
Post a Comment