TANGAZO


Monday, March 13, 2017

Wapiganaji wa IS waliosalia Mosul kuuawa, balozi wa Marekani McGurk asema


NablusHaki miliki ya pichaAFP
Image captionWanajeshi wa Iraq sasa wanadhibiti maeneo ya mashariki mwa Mosul

Mwanabalozi wa Marekani anayehusika katika kuongoza operesheni ya pamoja na ya majeshi dhidi ya wapiganaji wa Islamic State (IS) nchini Iraq amesema wapiganaji wa kundi hilo waliosalia mjini Mosul watauawa.
Brett McGurk, ametoa onyo hilo baada ya wanajeshi wa Iraq kuteka njia pekee iliyokuwa ikitumiwa na wapiganaji hao kuondoka au kuingia mji huo.
Hii ina maana kwamba wapiganaji wa kundi hilo waliosalia mjini humo wamekwama.
Wapiganaji wa IS wamedhibiti mji huo wa pili kwa ukubwa nchini Iraq tangu 2014.
Lakini wanajeshi wa Iraq wamefanikiwa kuteka maeneo makubwa ya mji huo katika operesheni ya kijeshi iliyodumu kwa miezi kadha.
Kwa sasa, wanajeshi hao, wakisaidiwa na Marekani, wamefanikiwa kudhibiti maeneo yote ya mashariki mwa mji huo, kupitia vita hivyo vilivyoanza Machi 5.
Wamefanikiwa pia kuwafurusha wapiganaji hao kutoka sehemu muhimu upande wa magharibi wa mji huo, ikiwa ni pamoja na makao makuu ya baraza la mji pamoja na makumbusho makuu ya Mosul.
Mapigano makali yaliendelea mwishoni mwa wiki, na Bw McGurk aliwaambia wanahabari mjini Baghdad Jumapili kwamba usiku wa kuamkia siku hiyo, wanajeshi wa Iraq walifanikiwa kuteka barabara ya mwisho iliyokuwa inadhibitiwa na IS.
Aliongeza: "Wapiganaji waliosalia Mosul, watauawa mjini humo, kwa sababu wamekwama sasa."
"Kwa hivyo, tumejitolea sio tu kuwashinda wapiganaji hao Mosul, bali pia kuhakikisha hawawezi kutoroka.
Meja Jenerali Maan al-Saadi, mkuu wa kikosi cha wanajeshi wa Iraq cha kukabiliana na ugaidi, alisema wanajeshi wa serikali sasa wanadhibiti zaidi ya theluthi moja ya magharibi mwa Mosul.
Alisema anaamini mapigano yatakuwa rahisi kuliko mashariki mwa Mosul, vita ambavyo vilichukua siku 100 kukamilika.
Mapigano yalianza Oktoba na wanajeshi wa Iraq wakafanikiwa kushinda IS mwezi Januari.

Map of Mosul city, 7 March 2017

No comments:

Post a Comment