Miili zaidi imetolewa kutoka kwa taka nyingi kwenye mji mkuu wa Ethiopia Addis Ababa, ambapo karibu watu 50 waliuawa wakati wa maporomoko ya taka mwishoni mwa wiki.
Oparesheni kubwa ya uokoaji kwa sasa inaendelea huku mamlaka zikihofia kuwa idadi ya waliokufa huenda ikaongezeka zaidi. Watu kadha bado hawajulikani waliko kufuatia mkasa huo.
Waokoaji wanatumia matingatinga na hata mikono yao kuondoa mawe na vifusi, wakati shughuli ya kuwatafuta manusura na wale waliokufa ikiendelea.
Waziri wa habari nchini humo Dr Negeri Lecho, anasema kuwa manusura wote watahamishiwa eneo lingine. Hadi sasa karibu familia 200 zimehamishwa.
Watu ambao walijeruhiwa wakati wa ajali hiyo ya siku ya Jumamosi wametibiwa na kuruhusiwa kuenda nyumbani.
Bado haijulikani kilichosababisha kuporomoka kwa taka hiyo lakini waziri mkuu nchini Ethiopia, ametuma rambi rambi zake kwa familia zilizoathiriwa akisema uchunguzi wa mkasa huo utafanyika.
No comments:
Post a Comment