Ripoti kutoka kambi ya wakimbizi ya Dadaab, iliyo kaskazini mashariki mwa Kenya, inasema kuwa walimu wawili raia wa Kenya wametekwa nyara.
Walimu hao walivamiwa manyumbani mwao na watu wenye silaha na wanaaminiwa kusafirishwa kuenda mpaka wa Somalia.
- Kenya: Mahakama yapinga hatua ya kufunga kambi Dadaab
- Kenya yalaumiwa kwa kukiuka sheria za wakimbizi
Walimu hao wanatajwa kuwa wasio na asili ya Somalia na walikuwa wakifunza kwenye shule moja ya kibinafsi iliyo kambi ya wakimbizi ya Hagardheere ambayo ni moja ya kambi za Dadaab.
Kisa hicho hata hivyo hakijathibitishwa rasmi.
Serikali ya Kenya ilitangaza kuwa inafunga kambi hiyo kutokana na sababu za kiusalama.
Hata hivyo mahakama kuu ya Nairobi, hivi majuzi iliamuru kuwa hatua hiyo ilienda kinyume na katiba na ukiukaji wa haki kwa karibu watu 300,000 kambini humo.
No comments:
Post a Comment