Mahakama ya Zimbabwe imepiga marufuku adhabu ya kuwachapa watoto shuleni na hata nyumbani .
Uamuzi huo unajiri baada ya mzazi mmoja kulalamika kwamba mwanawe katika darasa la kwanza alikuwa na majeraha mabaya baada ya kuchapwa na mwalimu.
Linah Pfungwah alisema kuwa mwanawe aliadhibiwa kwa kushindwa kutoa kitabu chake kwa wazazi kutiwa saini kama thibitisho la kwamba alifanya kazi yake ya shule.
Mahakama ya katiba inatarajiwa kuthibitisha uamuzi huo.
Mwandishi wa BBC Shingai Nyoka katika mji mkuu wa Harare anasema kuwa iwapo uamuzi huo utathibitishwa utabadilisha vile wazazi wanavyowaadhibu wanawao kwa karne kadhaa katika taifa hilo la Afrika ya kusini.
Baadhi ya wazazi wanakosoa uamuzi huo, huku makundi ya haki za kibinaadamu yakisema ulitarajiwa.
No comments:
Post a Comment