Mwanasheria mkuu nchini Marekani jenerali Jeff Sessions alikutana na balozi wa Urusi wakati wa uchaguzi licha ya kuthibitisha kuwa hakufanya mawasiliano yoyote na Urusi.
Idara ya haki ilithibitisha kuwa alikutana na Sergei Kislyak mnamo mwezi Julai na Septemba mwaka uliopita ikiwa ni miongoni mwa majukumu yake katika kamati ya bunge la seneti ya huduma za usalama.
- Ushahidi kuchunguza uchaguzi wa Marekani
- CIA kuchunguza iwapo Urusi ilingilia uchaguzi wa Marekani
- Trump akejeli madai kuwa Urusi ilivuruga uchaguzi
Bw Session alisema kuwa matamshi yake yalifananishwa na jukumu lake katika kampeni ya rais Trump.
Madai ya Urusi kuingilia uchaguzi wa Marekani yamemkabili rais Trump.
Idara ya ujasusi inaamini kwamba udukuzi unaodaiwa kufanywa na Urusi dhidi ya mgombea wa chama cha Democrat Hillary Clinton ulifanywa ukiwa na lengo la kumsaidia bw Trump kumshinda Clinton.
Mshauri wa maswala ya usalama wa rais Trump Michael Flynn alifutwa kazi mwezi uliopita baada ya kuidanganya ikulu kuhusu matamshi yake na bw Kislyak, kuhusu vikwazo dhidi ya Urusi
No comments:
Post a Comment