Rais wa Korea Kusini aliyetimuliwa mamlakani Park Geun-hye, ameondoka rasmi katika Ikulu ya Rais mjini Seuol, baada ya mahakama ya nchi hiyo kumvua wadhfa wa urais kutokana na kashfa ya kupotea kwa mabilioni ya pesa chini ya utawala wake.
- Mahakama yamng'atua mamlakani rais wa Korea Kusini
- Wabunge wapiga kura kumfuta rais wa Korea Kusini
- Korea Kaskazini yasema inajiandaa kushambulia Japan
Bi Park alindoka ikuli ambayo inafahamika kama Blue House leo Jumapili, baada ya kuwapa kwaheri wahudumu wake.
Msafara mkubwa ulimsafirisha kuenda nyumbani kwake katika wilaya ya Samseong.
Mamia ya wafuasi wake walikuwa wakimsubiri huko huku karibu polisi 1000 wakitumwa.
Hwang Kyo-ahn, ambaye ni mtiifu kwa Bi Park sasa ndiye kaimu Rais.
Tume ya uchaguzi nchini humo inasema kuwa uchaguzi ulio huru na wa haki utafanyika ifikapo tarehe 9 mwezi Mei.
Maelfu ya watu walimiminika barabarani mjini Seoul siku ya Jumamosi kusherehekea kuondoka kwa Bi Park, huku umati mkubwa wa wafuasi wake nao ukikusanyika eneo tofauti.
No comments:
Post a Comment