Nchini Marekani, muendesha mashtaka wa jimbo la Manhattan, amefutwa kazi na Rais Donald Trump.
Preet Bharara, ni mmojawepo wa waendesha mashtaka 46 walioteuliwa na Rais Baraack Obama, na ambao walishauriwa na Naibu Mwanasheria Mkuu kujiuzulu.
Bwana Bharara, alikataa kujiuzulu, baada ya kuambiwa binafsi na Trump, kusalia kwenye cheo chake muda mfupi baada ya uchaguzi mkuu wa Urais mwezi Novemba.
- Trump atia sahihi amri mpya ya kuzuia wahamiaji
- Jaji akataa kutoa uamuzi wa kupinga marufuku ya usafiri US
- Trump lawamani kuhusu matokeo Marekani
Kupitia mawasiliano ya mtandao wa kijamii wa Twitter, Bwana Bharara, ameelezea kinaga ubaga kuwa, hajajiuzulu bali amefutwa kazi.
Amezungumzia swala la kuwa muendesha mashtaka mkuu huko Manhattan, kama hatua kubwa kwa taaluma.
No comments:
Post a Comment