TANGAZO


Sunday, March 12, 2017

Polisi Afrika Kusini wampata mtoto wa mwezi mmoja aliyetoweka

Mtoto msichana mwenye umri wa mwezi mmoja, aliyetekwa nyara ndani ya gari huko Durban, Afrika KusiniHaki miliki ya pichaSOUTH AFRICAN POLICE SERVICE
Image captionMtoto msichana mwenye umri wa mwezi mmoja, aliyetekwa nyara ndani ya gari huko Durban, Afrika Kusini
Polisi nchini Afrika Kusini wanasema kuwa mtoto mchanga aliyekuwa ametekwa nyara ndani ya gari la mamake siku ya Ijumaa mjini Durban, amepatikana akiwa salama
Watu watatu wamekamatwa kuhusiana na uhalifu huo.
Msemaji wa polisi katika eneo la KwaZulu-Natal Luteni-Kanali Thulani Zwane, amethibitisha kuwa mtoto huyo alipatikana usiku wa manane kuamkia Jumapili.
Polisi walikuwa wakifuatilia vidokezo, ambapo baadaye viliwafanya kumpata ndani ya gari lililokuwa limeegezwa nje ya jumba la Mariannhill Toll Plaza.
Mtoto huyo wa mwezi mmoja anafahamika kama Siwaphiwe Mbambo.
Tangu siku ya Ijumaa polisi wamekuwa wakimtafuta mtoto mmoja aliyetoweka, baada ya gari la familia yao kutekwa nyara katika eneo la Durban.
Kisa hicho cha utekaji kiliwashtua watu wengi nchini humo na kuwafanya maelfu ya watu kutuma ujumbe kwenye mitandao ya kijamii ya Twitter kutoa habari aliko mtoto huyo.
Mtoto huyo mwenye umri wa mwezi mmoja, Siwaphiwe Mbambo, alikuwa katika kiti cha nyuma cha gari la mamake, pale gari hilo lilipotekwa na wanaume wawili waliokuwa na silaha nje ya duka moja kubwa la kununua bidhaa.
Gari jeupe muundo wa Toyota Yaris, lilipatikana baadaye na polisi likiwa limeachwaHaki miliki ya pichaMARSHALL SECURITY/FACEBOOK
Image captionGari jeupe muundo wa Toyota Yaris, lilipatikana baadaye na polisi likiwa limeachwa
Mamake alimnyakuwa mwanawe wa kiume wa miaka minane, lakini majambazi hao walitoweka kwa kasi na gari hilo, huku mtoto huyo mchanga Siwaphiwe, akiwa ndani.
Gari hilo lilipatikana baadaye na maafisa wa polisi bila ya mtoto huyo.
Zaidi ya maafisa 100 wa polisi wamekuwa wakiendesha operesheni kali ya kumtafuta mtoto huyo, katika kampeini inayoendeshwa na vyombo vya habari ya mtoto kuibiwa nchini humo.
Watekaji nyara hao waliliendesha gari hilo kwa kasi, huku mtoto huyo mdogo akiwa bado ndani, maafisa wamesema.

No comments:

Post a Comment