Mratibu wa Ujenzi wa nyumba zinazojengwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Arch. Christina Shayo (wa kwanza kushoto), akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani, mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa nyumba katika eneo la Magomeni jijini Dar es Salaam.
Muonekano wa moja ya nyumba za wananchi zinazojengwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) katika eneo la Magomeni ikiwa katika hatua ya msingi, nyumba hizo zinatarajiwa kuhudumia kaya 656 zitakapokamilia Septemba mwaka huu.
Mafundi
wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), wakiendelea na ujenzi wa nyumba za
wananchi katika eneo la Magomeni. Nyumba hizo zinatarajiwa kuhudumia kaya 656
zitakapokamilia Septemba mwaka huu. (Imetolewa
na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano)
No comments:
Post a Comment