TANGAZO


Wednesday, March 1, 2017

SSRA YAZINDUA MFUMO MPYA WA KURAHISISHA MAWASILIANO

Afisa Mwandamizi wa TEHAMA wa Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), David Ngh’ambi, akizungumza na waandishi wa habari, leo jijini Dar es Salaam, kuhusu mfumo wa kupokea malalamiko kwa njia ya TEHAMA, ambao mteja hutumia simu yake ya 'smart phone' katika kuwasilisha malalamiko na pia kupata ufumbuzi wa masuala yake kutoka mamlaka hiyo. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Uhamasishaji wa SSRA, Sarah Kibonde Msika na kushoto ni Afisa TEHAMA wa mamlaka hiyo, Ernest Masaka.(Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com) 
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari, wakichukua taarifa kuhusu mfumo wa kupokea malalamiko kwa njia ya TEHAMA, iliyokuwa ikitolewa na viongozi wa mamlaka hiyo katika mkutano huo.  
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari, wakisikiliza ufafanuzi wa taarifa kuhusu mfumo wa kupokea malalamiko kwa njia ya TEHAMA, iliyokuwa ikitolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Uhamasishaji wa SSRA, Sarah Kibonde Msika.
Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Uhamasishaji cha Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Sarah Kibonde Msika akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari, kuhusu mfumo wa kupokea malalamiko kwa njia ya TEHAMA, wakati wa mkutano huo, leo jijini Dar es Salaam.
Afisa TEHAMA wa SSRA, Ernest Masaka (kushoto), akielezea jinsi ya kutuma malalamiko kwa njia ya simu, wakati wa mkutano huo na waandishi wa habari leo, jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Uhamasishaji cha Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Sarah Kibonde Msika akiwaonesha waandishi wa habari, moja ya vipeperushi vyenye maelezo kuhusu mfumo wa kupokea malalamiko kwa njia ya TEHAMA pamoja na njia nyingine za mawasiliano na mamlaka hiyo.
Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Uhamasishaji cha Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Sarah Kibonde Msika akijibu maswali mbalimbali yaliyoulizwa na waandishi wa habari, kuhusu mfumo huo pamoja na mambo mengine kuhusu mamlaka hiyo.
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari, wakipata ufafanuzi kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Uhamasishaji wa SSRA, Sarah Kibonde Msika (kulia), kuhusu mfumo wa kupokea malalamiko kwa njia ya TEHAMA, ambao mteja hutumia simu yake ya 'smart phone' katika kuwasilisha malalamiko na pia kupata ufumbuzi wa masuala yake kutoka mamlaka hiyo.

Na Georgina Misama – Maelezo
MAMLAKA ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) imeanzisha mfumo wa TEHAMA utakaowawezesha wanachama kutuma na kufuatilia malalamiko yao moja kwa moja kwa mamlaka hiyo.

Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mkuu wa Kitengo Cha Mahusiano na Uhamasishaji kutoka mamlaka hiyo, Sarah Kibonde alisema Mfumo huo utaiwezesha SSRA kupokea na kushughulikia malalamiko ya wanachama moja kwa moja.

“Mfumo huu unapatikana katika simu za mkononi (mobile app), unapatikana kwa watumiaji wa simu za mkononi zinazotumia mfumo wa android na unatambuliwa kwa jina la SSRA” alisema Sarah.

Akitoa maelezo ya namna ya kutumia mfumo huo, Afisa TEHAMA wa SSRA Bw.Ernest Masaka alisema mara baada ya mwanachama kuingiza taarifa zake ambazo ni majina matatu, anwani ya posta, namba ya simu, pamoja na namba ya uanachama na makazi, mfumo utampa namba ya kumbukumbu ya lalamiko husika.

Aidha, taarifa hizi husaidia kumtambua muhusika na Mamlaka kufanya mawasiliano na mwanachama mwenye malalamiko pamoja na kushughulikia malalamiko husika moja kwa moja. 

“Mfumo huu umeweka utaratibu wa mlalamikaji kufuatilia  hatua za utatuzi wa malalamiko yake kwa kumbukumbu za mlalamikaji” alisema Bw.Masaka.
   
Akizungumzia faida zinazopatikana kwa wanachama kutumia mfumo huo Bw.Masaka alisema ni pamoja uwekaji mzuri wa kumbukumbu kwa Mamlaka,kutoa mrejesho wa idadi na hatua za utekelezaji pamoja na mwanachama kupata mrejesho kwa haraka bila kujali mahali alipo ambayo itasaidia kupunguza ghara za fedha na muda.

Mamlaka inatoa wito kwa wanachama na wananchi wote kwa ujumla kutumia mfumo huu kwasababu unarahisisha mawasiliano kati ya mlalamikaji na Mamlaka.

No comments:

Post a Comment