TANGAZO


Sunday, January 22, 2017

Waziri Mkuu wa Mauritius kumkabidhi mwanawe madaraka

Bwana Jugnauth amekuwa kwenye siasa za Mauritius kwa miongo kadha

Haki miliki ya pichaAFP
Image captionBwana Jugnauth amekuwa kwenye siasa za Mauritius kwa miongo kadha
Waziri Mkuu wa Mauritius Anerood Jugnauth anasema anaoandoka madarakani na kumkabidhi mwanawe Pavind madaraka.
Waziri huyo mkuu mwenye umri wa miaka 82 alichukua wadhifa kwanza mwaka 1982.
Katika tangazo kwa njia ya runinga bwana Jugnauth anasema anajiuzulu ili kutoa nafasi kwa kiongozi mwenye umri mdogo na mwenye nguvu.
Mwanawe kwa sasa ni waziri wa fedha. Vyama vya upinzani vimekosoa hatua hiyo lakini hakuna kile vitafanya kuzuia hatua hiyo.
Jugnauth ni mkuu wa chama kikubwa ziadi katika muungano unaoongoza.
Mauritius, nchi iliyo habari ya Hindi ni koloni ya zamani ya Uingereza. Atakabidhi mwanawe madaraka Jumatatu asubuhi.

No comments:

Post a Comment