Siku moja baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kuchukua hatamu y a uongozi wa taifa hilo, amelaamu baadhi ya vyombo vya habari kwa kueneza taarifa za uongo juu ya idadi ya watu waliyohudhuria sherehe ya kuapishwa kwake.
Trump amesema zaidi ya watu milioni moja walihuthuria shere hiyo.
Msemaji wa White House, Sean Spicer, amesema vyombo hivyo vya habari vinaendesha kampeini ya kugawanya watu kwa kuangazia habari ambazo hazina msingi wowote.
Hata hivyo kanda za video za matangazo ya moja kwa moja wakati wa hafla hiyo hazikunasa umati mkubwa wa watu.
Picha zinaonekana zikionyesha watu wengi waliohudhuria shereha ya kupishwa kwa rais Barack Obama mwaka 2009.
Bwana Trumpo hakuzungumzia maandamano wakati alitembelea makao makuu ya CIA jimbo la Virginia siku ya Jumamosi, lakini badala yake alishambulia vyombo vya habari.
Bwana Trump alisema kuwa video na picha wakati wa kuapishwa kwake zilionyesha taarifa ziziso za ukweli.
"Walionekana kama watu milioni 1.5 siku nya Ijumaa, alisema Trump, na kuzua ripoti za vyombo vya habari kuwa walikuwa watu chini ya 250,000.
Rais huyo mpya aliwataja waandishi wa habari kuwa watu waongo zaidi duniani.
No comments:
Post a Comment