TANGAZO


Sunday, January 22, 2017

WATANZANIA WAHIMIZWA KUZINGATIA USAWA WA KIJINSIA KATIKA SEKTA YA KILIMO

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Sehemu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya umma –SJMC) Bw. Dotto Kuhenga akionyesha waandishi wa habari kitabu cha mwongozo wa waandishi wa habari katika utekelezaji wa mradi wa uhamasishaji usawa wa kijinsia katika kilimo, uhakika wa chakula na lishe leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo LAND O’ LAKES Dkt. Rose Kingamkono na Mtafiti kutoka Taasisi ya Taaluma ya Maendeleo UDSM Profesa Bertha Omari Koda (kulia). 
Mtafiti kutoka Taasisi ya Taaluma ya Maendeleo ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Profesa Bertha Omari Koda akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati wa mkutano wao na waandishi hao(hawapo pichani) kuhusu mradi wa uhamasishaji usawa wa kijinsia katika kilimo, uhakika wa chakula na lishe leo jijini Dar es Salaam.Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo LAND O’ LAKES Dkt. Rose Kingamkono na Mtaalamu Mwelekezi wa masuala ya Jinsia,Utawala Bora na Maendeleo kutoka LAND O’ LAKES Bibi. Margreth Henjewele. 
PIX2: Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo LAND O’ LAKES Dkt. Rose Kingamkono akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) kitabu kinachotumika kutoa elimu juu ya usawa wa kijinsia katika sekta ya kilimo, sheria za kimila leo jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Mhadhiri wa Shule Kuunya Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma (SJMC) Bw. Dotto Kuhenga, Mtafiti kutoka Taasisi ya Taaluma ya Maendeleo UDSM Profesa Bertha Omari Koda na Mtaalamu Mwelekezi wa masuala ya Jinsia,Utawala Bora na Maendeleo kutoka LAND O’ LAKES Bibi. Margreth Henjewele. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo LAND O’ LAKES Dkt. Rose Kingamkono akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mradi wa uhamasishaji usawa wa kijinsia katika kilimo, uhakika wa chakula na lishe leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mtafiti kutoka Taasisi ya Taaluma ya Maendeleo UDSM Profesa Bertha Omari Koda. 
Mtaalamu Mwelekezi wa masuala ya Jinsia,Utawala Bora na Maendeleo kutoka LAND O’ LAKES Bibi. Margreth Henjewele akitoa ufafanuzi kuhusu mradi wa uhamasishaji usawa wa kijinsia katika kilimo, uhakika wa chakula na lishe leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo LAND O’ LAKES Dkt. Rose Kingamkono.

No comments:

Post a Comment