Waimbaji wa Kwaya ya Kanisa la EAGT Kaangaye kutoka Nyakato Jijini Mwanza, leo wamefanyika Baraka kubwa baada ya kuhudumu vyema katika Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo nyuma ya Soko Kuu la Sabasaba, Ilemela Jijini Mwanza.
Waumini wengi wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya wamefurahishwa na huduma ya kwaya hiyo. Pongezi kubwa ziwaendee Mwenyekiti wa kwanya hiyo, Abednego Magesa na Mchungaji Samson Mniko kwa malezi mema yaliyofanikisha wanakwaya hao kumtumikia Mungu kwa bidii kubwa.(Na Binagi Media Group)
Waimbaji wa Kwaya ya Kanisa la EAGT Kaangaye lililopo Nyakato Jijini Mwanza, wakihudumu kwa bashasha kubwa kwenye ibada za hii leo jumapili katika Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo Sabasaba Ilemela Jijini Mwanza.
Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya, Dkt.Daniel Moses Kulola, akisisitiza jambo kwenye ibada za hii leo jumapili. Ibada ya kwanza kila jumapili huanza saa 12:00 asubuhi, ibada ya pili saa 01:00 asubuhi na ibada ya tatu saa 04:30 asubuhi.
Waumini wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo nyuma ya Soko Kuu Sabasaba Ilemela Jijini Mwanza, wakimsikiliza Mchungaji Kiongozi wa Kanisa hilo, Dk. Daniel Moses Kulola.
Waumini wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo nyuma ya Soko Kuu Sabasaba Ilemela Jijini Mwanza, wakifuatilia ibada za leo Jumapili.
Mahubiri na Mafundisho ya neno la Mungu kutoka Kanisa la EAGT Lumala Mpya pia yanarushwa kupitia runinga ya Star Religion inayopatikana kwenye kisimbuzi cha Continental ambapo visimbuzi hivyo vinapatikana kanisani hapo kwa punguzo kubwa. (Picha na Craty Cleophace @EAGT Lumala Mya)
No comments:
Post a Comment